BREAKING NEWS

Wednesday, July 27, 2022

HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA YAJIPANGA KUBORESHA SEKTA ZA UMEME BARABARA KUVUTIA UTALII

 Halmashauri ya Jiji la Arusha limejipanga kuboresha sekta za maji Umeme,barabara na usafi wa mazingira kwa kuandaa Baraza Maalum kujadili changamoto hizo ikiwa ni mkakati wa kuvutia utalii


Akiongea Wakati akifunga kikao cha Baraza la madiwani Mstahiki Meya wa Jiji hilo Maxmillian Iranqe amesema kuwa wametoa bilion mbili kwa Tarura kwa ajili ya utengenezaji na ukarabati wa barabara sanjari na mitambo.


Alisema kwamba pia wametenga kiasi cha milion 50 kwa ajili ya kuweka vitupio taka ndani ya Jiji hilo ambapo Amewataka wananchi kujenga tabia ya kutunza vifaa hivyo sanjari na Utamaduni wa kutotupa takataka holela.


"Kumejengeka mazoea wananchi wengi pindi tunapoweka vitupio taka wao kung'oa na kuuza chuma chakavu tunawaomba kujenga Utamaduni wa kuvitunza kwa ajili ya kuliweka Jiji letu katika hali ya Usafi ili kuvutia watalii"


Alisema kwamba Jiji hilo watakwti na Tanesco na Tarura kuona namna ya kuweka Taa zenye camera kuweza kusaidia ulinzi na usalama kwa wageni hususani Watalii hivyo hivyo katika sekta ya majisafi ili kuondoa kero na adha kwa wananchi wetu.


Awali Kaimu Mkurugenzi Jiji la Arusha Dkt. Onesmo Mandike ameeleza kwamba maagizo na maelekezo yote waliopewa katika Baraza hilo wataenda kuyafanyiakazi kuhakikisha Jiji linaongeza mapato yake kuweza kujiendesha.


Alisema uwekaji wa Taa zenye kamera kusaidia ulinzi na usalama ndani ya Jiji letu ni hatua nzuri ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais alietangaza Utalii ikizingatiwa Jiji letu ni kitovu cha Utalii. 



Alisema kwamba suala la soko la vitunguu eneo la Engutoto wanaenda kujipanga kuhakikisha maagizo yote wanayafanyia kazi haraka kuongeza chanzo cha mapato sanjari na kusimamia kuona mamlaka ya maji inatoa. 

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates