BREAKING NEWS

Wednesday, July 20, 2022

EAC IPO VIZURI KATIKA SOKO LA PAMOJA DKT. KIJAJI




 Jumuiya ya Afrika Mashariki ipo vizuri na inakuwa kiuchumi kwa kasi hivyo kila nchi itumie fursa za kibiashara kwa kufanyabiashara kutoka nchi Moja kwenda nyingine. 


Aidha Kuna vikwazo vya kikodi na visivyo kikodi kama mtakumbuka serikali ya awamu ya sita ilikuwa na vikwazo 68 na vikafanyiwa kazi na Sasa vimebakia 12

Akiongea katika Kongamano la Biashara la Afrika Mashariki kuelekea Kikao Cha wakuu wa EAC Kesho Waziri wa biashara na Uwekezaji Dkt. Ashatu Kijaji amesema serikali ya Tanzania imeongeza wigo wa kibiashara kati ya Mataifa ya Jumuiya hiyo ikiwemo kufungua biashara katika yake na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (DRC)

Alisema kwamba Soko huru la bidhaa ndani ya Afrika Mashariki limeanza kukuwa hivyo ipo haja kuendelea kuboresha na kuona namna ya kukabiliana na changamoto zinazolikabili ili kuwezesha faida baina ya nchi hizo.

"Kama mnavyoona tumepita katika mkwamo baada ya Uviko 19 tumeendelea kuboresha biashara baina ya nchi zetu kuondoa vikwazo vya kikodi na visivyo vya kikodi Lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya ufanyaji wa biashara baina ya nchi zetu" alisema Dkt. Kijaji.

Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara a Uwekezaji Prof. Godius Kahyarara amesema kwamba Soko la Tanzania limezidi kuongeza wigo na hivyo kuongeza mapato ya Kodi hadi asilimia 46 kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania.

Amesema kwamba biashara ndani ya nchi hizo imezidi kukua na kufikia Dola Bilion 10 kwa nchi zote za Afrika hivyo kuongeza fursa za kibiashara kutoka nchi Moja kwenda nchi nyingine.

"Kama serikali tumejipanga kuweza kuongeza na kutumia fursa za kibiashara ikiwemo bidhaa zetu kuuzwa katika Masoko ya nchi za wenzetu na kuzalisha faida pia kutokuwa wapokeaji wa bidhaa kwa kupunguza ununuzi kutoka nchi nyingine tofauti na awali

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates