Ticker

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TELEOLOGY AWATAKA VIONGOZI NA TAASISI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA SHULE KWA AJILI YA WANAFUNZI WENYE MAITAJI MAALUMU.

  


Naibu Waziri wa elimu sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga amewataka viongozi wa taasisi pamoja na wadau wanojishungulisha na utoaji wa elimu jumuishi  kuendelea kushirikiana na serikali katika kujenga  shule Kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

 Hata hivyo amesema serikali itaendelea kuweka msukumo mkubwa katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunza kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ikiwemo kuwezesha ujenzi na ukarabati wa miundombinu mbalimbali rafiki kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika ngazi zote za elimu.


Akizungumza katika uzinduzi wa shule Jumuishi ya mfano ya Patandi Sekondari iliyojengwa na Serikali kupitia Mradi wa Lipa kulingana na matokeo (EP4R), Naibu Waziri wa elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipinga amesema 

Amesema kuwa mbali na ukarabati huo vingine ni ununuzi na usambazaji wa vifaa vya kujifunza na kufundishia na vifaa saidizi vya kisasa  na vya kidigitali kwa ajili ya wanafunzi hao na mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu 1,947 wanaofundisha wanafunzi hao na kuandaa kamusi ya lugha ya alama ya Tanzania wka lengo la kurahisisha mawasiliano na ufundishaji na ujifunzaji.

"Serikali imeridhia matamko mbalimbali ikiwemo tamko la haki za watu wenye ulemavu,lengo ikiwa ni kuondoa vikwazo vyote vya kimfumo na kimuundo vinavyozuia kundi fulani la watanzania kupata haki ya elimu na kushiriki kikamilifu kujifunza na kumaliza elimu katika ngazi zote za elimu,"amesema

"Natoa wito kwa viongozi wa taasisi na wadau wanaojihusisha na utoaji elimu jumuishi kuendelea kushirikiana na serikali kujenga shule pia kuhamasisha umuhimu wa elimu kwa watu wenye mahitaji maalum ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa ujifunzaji,"

Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa mradi huo,Mkurugenzi Elimu Maalum na Jumuishi kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Dk Magreth Matonya,amesema ujenzi wa shule hiyo iliyogharimu zaidi ya Sh3.8 bilioni ulianza mwaka 2017.

Mkurugenzi huyo amesema shule hiyo imejengwa baada ya kuona changamoto wanayokutana nayo wanafunzi wenye ulemavu wa aina mbalimbali wanaosoma Sekondari hivyo kuweka miundombinj wezeshi kwa ajili ya makundi mbalimbali.

Dk Magreth amesema shule hiyo yenye madarasa 12 ina wanafunzi 288,mabweni manne ambapo kila bweni lina vyumba vinne vyenye miundombinu maalum kwa wanaotumia viti mwendo,maabara na nyumba za walimu siko kwenye hatua ya mwisho.

"Shule hii ni jumuishi ya mfano,inachukua wanafunzi wenye ulemavu wa aina mbalimbali na wasio na ulemavu wowote na awali,"alisema

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Carolyne Nombo,alisema shule hiyo jumuishi ya mfano ya Sekondari Patandi ni ya kitaifa katika ngazi hiyo na ya kipekee nchini.

Amesema shule hiyo imedahilo wanafunzi kutoka mikoa mbalimbali nchini na kuwa wamepokea ombi la kuanzisha shule nyingine katika Kanda mbalimbali ili ziwezeshe wanafunzi wengi kupata elimu kwenye mazingira ya karibu.

Kwa upande wake Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,serikali za mitaa-Tamisemi (Elimu),Dk Charles Msonde, alisema changamoto zilizoanishwa ikiwemo ujenzi wa shule jumuishi katika Kanda na kuwa wataangalia namna ya kuzifanyia kazi.

Awali Ofisa Elimu Mkoa wa Arusha,Abel Ntupwa,ameomba serikali kuongeza ujenzi wa shule jumuishi za mfano katika Kanda mbalimbali hapa nchini ili kusaidia kupatikana kwa huduma hiyo muhimu karibu na maeneo 

Post a Comment

0 Comments