BREAKING NEWS

Monday, July 18, 2022

MBARONI KWA KUMUUA KWA PANGA MFANYABIASHARA

 



MKAZI wa kijiji cha Mgombani ,wilaya ya Monduli Mkoani Arusha, Juma Ndaji(27) , anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani humo kwa kosa la kumkata panga mfanyabiashara ,Paulo Akwesso(58) na kumsababishia kifo chake akimtuhumu kuwa na mahusiano na mpenzi wake.

Aidha mtuhumiwa huyo pia alimjeruhi kwa panga mwanamke Rebeka  John (22)anayedsiwa kuwa ni mpenzi wake ambaye elazwa katika kituo cha Afya Mto wa mbu kwa matibabu,baada ya kumkuta na marehemu wamelala kitanda kimoja.

Akiongea na waandishi  wa habari Mkuu wa wilaya ya Monduli Frank Mwaisumbe alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa nne usiku  katika kitongoji cha Kirurumo, kata ya Majengo,katika chumba cha mwanamke huyo.

Akifafanua kuwa chanzo cha tukio hilo ni mtuhumiwa kumtuhumu marehemu  kuwa na mahusiano na mpenzi wake ambaye pia alijeruhiwa kwa panga baada ya kuwakuta wakijivinjari chumbani. 

Mwenyekiti wa kijiji cha Migombani ,Festo Philpo alisema kwamba mara baada ya kupata taarifa za tukio hilo alifika katika chumba cha Rebeka na kukuta polisi wakimhoji mtuhumiwa ambaye alikiri kuhusika kumshambulia marehemu na kumsababishia umauti.

Mwenyekiti huyo akifafanua  kuwa marehemu alikuwa akifanyabiashara ya kuuza vinywaji huku Rebeca akiwa mfanyakazi wake.

Alisema kuwa awali mtuhumiwa alikuwa na mahusiano na Rebeca lakini walitengana kitambo, hivyo hatua ya kuwenda kuwashambulia kwa Panga ni kutokana na wivu wa mapenzi.

Alisema kuwa mtuhumiwa alipata taarifa kuwa Marehemu amekuwa akienda kstika chumba cha Rebeka na kulala ndipo alipoamua kumvizia usiku akiwa na panga mkononi na kufanikiwa kuwakuta.

"Mtuhumiwa alifika katika chumba cha Rebeka na kumkuta marehemu akiwa chumbani na kuanza kumkata na panga na kuwajeruhi wote wawili lakini marehemu Paulo alivuja damu nyingi sana na kufariki dunia akipatiwa matibabu katika kituo cha afya mto wa mbu ''Alisema 

Alisema marehemu alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika kituo cha Afya Mto wa Mbu baada ya kuvuja damu nyingi na polisi inamshikilia mtuhumiwa kwa kusababisha kifo cha marehemu. 

Hata hivyo aliongeza kuwa mtuhumiwa baada ya tukio hilo alijitahidi kuficha Panga kwa kulitupa kwenye shamba la migomba, lakini polisi walifanikiwa kulipata likiwa katikati ya mgomba likiwa na damu mbichi.

Mwili wa marehemu  umehifadhiwa katika kituo cha Afya Mto wa Mbu ukisubiri uchunguzi wa daktari ,mtuhumiwa ambaye anashikiliwa polisi atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za mauaji zinazomkabili.


Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates