BREAKING NEWS

Thursday, July 28, 2022

MAMLAKA ZA BIMA PAMOJA NA WADAU WATAKIWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSIANA NA BIMA

 Mamlaka ya Bima Tanzania pamoja na wadau wote wametakiwa kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kuwa na uwelewa wa kutosha kuhusu bima

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella alipomuwakilisha Waziri wa fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Nchemba katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa washauri na madalali wa bima Tanzania.

Amesema uimarishaji wa mifumo ya upatikanaji wa huduma za bima kwa wananchi wengi ni kujenga uelewa kuhusu umuhimu wa huduma hizo.



Huduma ya bima  ni chachu kubwa ya mafanikio kwa tasnia ya bima yenyewe na nchi kwa ujumla.

Amesisitiza kuwa elimu hiyo iwafikie hata wananchi wanaoishi vijijini ili wafahamu umuhimu wake na waweze kujiunga kwa wingi.

Aidha, ameiagiza mamlaka ya bima Tanzania kuandaa mjadala maalumu wa wadau wa bima wakujadili namna ya kuimarisha sheria,kanuni, taratibu na miongozo ya kusimamia biashara ya bima nchini ili kutengeneza fursa za wawekezaji katika tasnia hiyo.

Changamoto iliyopo kwa sasa ni uchache wa makampuni ya bima  mtawanyo nchini, hivyo mamlaka ya bima ione namna ya kutengeneza mazingira bora ya kuvutia wawekezaji.

Uwekezaji wa ndani utasaidia  uwezo wa ndani wa soko la bima na hata pia katika pato la Taifa kwani kwa Sasa mauzo ghafi yanayobaki nchini ni 60%.

Mkutano huo unafanyika kwa siku mbili ukiwa umejumuisha washauri na madalali wa bima Tanzania

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates