ZIARA
za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
kwenye mataifa mbalimbali duniani zimezaa matunda kwa kufanya idadi ya
wawekezaji nchini kuongozeka.
Rais
Samia amekua akiwahakikishia wawekezaji kutoka nje kuja nchini kwani
kuna mazingira mazuri ya uwekezaji na pia malighafi zote zinatohitajika
katika shughuli za uwekezaji.
“Ndugu
zangu mabibi na mabwana, serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi
na rafiki kwa ufanyaji wa biashara na uwekezaji. Tunafahamu bila mchango
wa sekta binafsi hatuwezi kuleta mageuzi makubwa ya uchumi wa nchi
yetu.” - Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
Pia,
Rais Samia ameshawishi wawekezaji wengi kuja kuwekeza nchini kupitia
filamu ya Royal Tour Tanzania ambapo ndani yake Mkuu huyu wa nchi
ameonyesha vivutio vingi vinavyopatikana Tanzania hivyo kuzidi kuvutia
wageni kuja kuwekeza nchi kwenye sekta ya utalii.
Hivi
sasa, takwimu zinaonyesha kwamba idadi ya watalii wanaoingia nchini
hususani jijini Dar es Salaam imeongezeka kwa asilimia 280 na Arusha
asilimia 340 na hii ni kutokana na namna Rais Samia Suluhu
anavyojitahidi kunadi utalii na vivutio vilivyopo nchini.
Tayari
wawekezaji wameanza kuja nchini na kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali
huku Rais Samia alihamasisha kuonyesha ushirikiano kwao pindi
wanapoonyesha nia ya kuja kuwekeza kwani kupitia wao ajira zitazalishwa
na pia kubadilishana ujuzi wa mambo mbalimbali.
Baada
ya kumalizikina kwa maonyesho ya sabasaba mwaka huu 2022, ilisainiwa
mikataba 19 na wawekezaji waliotembela maonyesho hayo kutoka mataifa
mbalimbali.
Mikataba
10 ya ujenzi wa viwanda vikubwa 500 vya kuchakata nafaka, kuuza na
kununua mazao, ufugaji samaki, usafirishaji bidhaa kimataifa
utakaokamilika mwaka 2025.
Mikataba 9 ya uwekezaji wa eneo maalum la viwanda la Sino Tan Park ambavyo ni Kwara vilivyopo Kibaha mkoani Pwani.
Viwanda hivyo vitazalisha ajira 500,000 ambapo 100,000 ajira za moja kwa moja na 400,000 za muda.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia