Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI KUFANYA MABORESHO KATIKA HOSPITAL YA TAIFA MUHIMBIILI


 Dar es salaam

Serikali itafanya maboresho makubwa katika  miundombinu ya kutolea huduma ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kujenga majengo mapya yatakayorahisisha hali ya utoaji huduma ili kutimiza nia ya serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha huduma za kibingwa zinapatikana nchini.


Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Ndg. Shaka Hamdu Shaka wakati alipofika hospitalini hapo kujionea hali ya utoaji huduma.


Ndugu Shaka amesema kuwa nia ya Serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa nchini kuanzia ngazi  ya msingi hadi taifa.


“Hospitali ya Taifa Muhimbili inafanya kazi nzuri sana, tofauti na inavyosemwa huko nje, kwa nyakati tofauti serikali za awamu zote zimejitahidi kuwekeza kwenye sekta ya afya hadi kufikia sasa huduma nyingi za kibingwa zinafanyika hapa nchini, changamoto kubwa ya hospitali hii ni uchakavu wa miundombinu kwa kuwa majengo mengi yaliyopo yalijengwa kati ya miaka 70-100 iliyopita” amesema Ndg. Shaka


Aidha amepongeza jitihada mbalimbali ambazo uongozi wa hospitali umekuwa ukizifanya katika kukabiliana na changamoto ya uchakavu wa miundombinu ikiwemo kufanya ukarabati wa mara kwa mara.


Katika hatua nyingine Ndg. Shaka amepongeza wataalamu MNH walioshiriki katika upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha mapacha walioungana uliofanyika Julai Mosi mwaka huu.


Naye Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa MNH Bi. Zuhura Mawona,  akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji amesema kuwa hospitali katikakipindi cha mwaka mmoja wa serikali ya awamu ya sita hospitali imeendelea kutoa huduma za kibingwa ikiwemo upandikizaji Figo, upandikizaji Uloto, upandikizaji wa vifaa vya kusaidia kusikia pamoja na tiba Radiolojia.

Post a Comment

0 Comments