W
Jenerali Michael Mumanga Akizungumza na wadau wa maafa jijini Arusha.
Ofisi ya Waziri Mkuu katika
kutekeleza Sheria ya usimamizi wa maafa imeànza kuimarisha uratibu wa
shughuli za udhibiti wa maafa kwa kuhakikisha uwepo wa mfumo thabiti
katika ngazi Zote
Katika ufunguzi wa jukwaa la Wadau wa udhibiti
wa maafa kwa ajili ya kujadili na kudhibitisha mpango wa Taifa wa
kujiandaa na kukabiliana na maafa na mkakati wa mawasiliano wakati wa
dharura uliowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya maafa jijini Arusha
Mkurugenzi
idara ya menejiment ya maafa kutoka Ofisi ya waziri Mkuu Meja Jenerali
Michael Mumanga,anasema lengo la jukwaa hili Ni kutoa fursa kwa Wadau
kutoa maoni yao kwa lengo la kuboresha na kuthibitisha mpango
ulioandaliwa
Jenerali Mumanga anasema kutokana na kuongezeka kwa
matukio ya majanga ambayo yamekuwa yakisababisha maafa,serikali kwa
kushirikiana na wadau wameona Ni muhimu kuwa na mipango mikakati yenye
lengo la kujiandaa na kupunguza vihatarishi vya maafa
"Mipango
hii mikakati ni kuhakikisha kuwa pindi maafa yanapotokea ni namna gani
nchi itawajibika katika kutatua au kupunguza maafa hayo" Alisema
jenerali
Kwa upande wao Wadau wa maendeleo wanasema kukutana kwa
wataalam Hawa Kuna lengo la kupitia na kujadili namna ya kupunguza
athari za majanga
Mpango huu wa Taifa wa kujiandaa na kukabiliana
na maafa ulianza mwaka 2012 ukizishirikisha Taasisi za kiserikali na
zisizo za kiserikali.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia