Na Ahmed Mahmoud
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha John Mongela ameionya Halmashauri ya Arusha DC kuacha
utegenezi wa fedha kutoka serikali kuu na kujikita kuongeza mapato ya
Halmashauri hiyo.
Mongela
Ameyasema hayo kwenye Kikao Maalum cha Baraza la Madiwani kujadili hoja
za Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali kilichofanyika kwenye ukumbi wa
Halmashauri hiyo.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Mkoa Kwa miezi mitatu serikali kuu isipoleta fedha
Halmashauri hiyo inaweza kufungwa tafsiri halisi ya CAG asilimia 87
inatoka serikali kuu ambapo Halmashauri hiyo uwezo wake ni asilimia 13
Alisema
kwamba Halmashauri ijadili jinsi ya kujenga uwezo wa mapato yake ya
ndani kwa kuwa ni mzigo na haikutakiwa kuwepo Kutokana na utegenezi wake
kwa serikali kuu.
"Hii
ni Tafsiri ya Mkaguzi Mkuu wa serikali CAG uwezo wa halmashauri kuhimili
kujiendesha ni asilimia 13 tu na utegemezi wake kwa serikali kuu ni
asilimia 87 serikali ikiamua kutoleta fedha kwa miezi mitatu hamna
Halmashauri kwa Tafsiri rahisi ni mzigo"
Aidha
Mongela amesema kwamba Kwa kuwa ni wajibu wa kimsingi wa kikatiba
kugatua madaraka ndio maana serikali kuu inawajibu wa kutafuta fedha za
Kuendesha Halmashauri hiyo waheshimiwa madiwani uwezo wetu upo chini
Halmashauri Ina uwezo wa kuongeza mapato maelekezo yapo kaeni chini
kuongeza mapato
Alisema
Ukitizama huku ndani ni mfumo Mkurugenzi ni kazi yako kuwa mbunifu
vyanzo ni vile vile hakuna Ubunifu na matokeo yake hata fedha
zinazoletwa mahitaji yanazidi hakuna Ubunifu uwezo ni mdogo na matokeo
yake unapeleka kwenye sehemu nyingine
Amesema
kwamba Mwenyekiti itisha kikao kujua miradi inayobuniw na kutelezwa
ndani ya Halmashauri hii uone kama Kuna fedha za ndani zaidi ya fedha
hizi za serikali kimsingi hatuna uwezo wa kimapato lakini tuna uwezo
mkubwa wa kuanzisha mapato
"Mkurugenzi
Huna vyanzo vipya vyanzo vilevile na vyanzo vilivyopo vimepitwa na
hakuna Ubunifu hivyo hakuna uwezo wa mapato, hamna uwezo wa mapato
uwezo ni mdogo vyanzo vipo vingi vyanzo ni viwili tu vya soko la karoti
haiwezekani acheni urasimu"
"Kwenye
mambo ya Msingi kupishana sioni tatizo Lengo liwe kuongeza mapato
kubuni vyanzo vipya hivyo nisisitize suala la kujenga mapato ya
Halmashauri lakini kwenye hoja hizi zipo za kizamani hakuna kitu kigumu
kama umaskini ila nyie ni malofa"
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia