Picha
ikionyesha wachezaji wa timu ya taifa ya Taekwondo pamoja na kocha wa
timu hiyo ya taifa mwenyewe asili ya kichina walioenda kuwakilisha
nchi katika mashindano ya kusaka ubigwa wa mchezo wa Taekwondo Afrika
yanayofanyika yanayo tarijiwa kuanza kutimua vumbi July 13 hadi 17
mwaka huu nchini Rwanda (picha na Woinde Shizza)
Na Woinde Shizza ARUSHA
Timu
ya taifa ya mchezo wa Taekwondo imeondoka leo nchini kueleekea nchini
Rwanda kwa ajili ya kushiriki mashindani ya ubigwa wa mchezo huo kwa
nchi za afrika yanayoa yanayotarajiwa kuanza July 13 hadi 17 nchini
humo.
Akiongea na
waandishi wa habari mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la Taekwondo
Tanzania Richard Kitolo alisema kuwa timu ya taifa ya mchezo huo
inatarajiwa kuondoka leo July kwenda nchini Rwanda kwa ajili ya
kushiriki mashindani ya kusaka ubigwa wa Afrika wa mchezo huo.
Alisema
kuwa katika mashindani hayo nchi 40 kutoka afrika zimethibitisha
kushiriki mashindano hayo yatakayo fanyika katika uwanja wa Arena
Kigali nchini Rwanda,huku akibainisha kuwa jumla ya wachezaji wanne na
viongozi wawili wanatarajiwa kuondoka kwenye msafara huo
Akibainisha kuwa maandalizi yamekamilika na wachezaji wote wapo vizuri kwa ajili ya kwenda kushiriki mashindano hayo.
Kwa
upande wake kocha mkuu wa timu ya taifa ya Taekwondo Kim Keumloon
alisema maandalizi ya wachezaji yamekamilika na wamefanya mazoezi
yakutosha na wanaimani watakuja na ushindi
"Tumefanya
mazoezi kwa kadri ya uwezo wetu tunaamini tutashinda na kuleta ushindi
nyumbani na kuletea ushindi nchi ,japo tunajua timu kule kuna Kuna timu
zilizofanya mazoezi yakutosha lakini nina amini tutashinda a nazo na
tutarudi na medali "alisema
Naye
kocha mchezaji wa timu hiyo David Saimoni alisema kuwa wakati wanaenda
kuiwakilisha nchi katika mashindano haya awajapata msaada wowote kutoka
serikali hivyo wameiomba serikali kuwapa msaada na kuukumbuka mchezo
huu kama vile wanavyokumbuka na kuthamini mchezo mpira wa miguu.
"Tunaiomba
serikali iukumbuke na mchezo huu iweze kuupa ruzuku kama vile inavyotoa
kwa michezo mingine kama mpira wa miguu,katika mashindano haya
atujapewa msaada wowote kutoka serikali ila tunaenda kuiwakilisha nchi
sisi tunachoomba watukumbuke na sisi tunamashindano mwezi wa tisa
tulikuwa tunaomba msaada wao"alisema
Alitaja
wachezaji wanaoenda kushindana katika mchezo huu kuwa ni Danny
Mkaima,Erick Kaguri ,Ramadhani Msafiri pamoja na David Samson
Akibainisha
kuwa wanapoenda katika mashindano haya wanaimani watakuja na ushindi
mkubwa kwani wamejiandaa vyema na wanaenda kushindana na sio kutalii
ivyo wanaimani watakuja na ushindi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia