BREAKING NEWS

Thursday, July 28, 2022

UMEFIKA WAKATI WA KILA DIWANI KUJITAFAKARI NA KUFANYAKAZI KWA BIDII ILI KUWEZA KUTATUA KERO ZA WANANCHI:ME YA WA JIJI LA ARUSHA MAXIMILIAN

 Baraza la Madiwani wa jiji la Arusha limemchagua kwa mara nyingine Diwani wa Viti Maalum (CCM), Veronica Mwelange kuwa naibu meya wa jiji hilo ambapo amepata kura zote 32 zilizopigwa na madiwani hao.



Katika kikao hicho cha baraza la madiwani Julai 28, 2022, Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iraghe alisema kuwa, naibu meya amepita baada ya jina lake kupitatishwa ndani ya chama chake cha CCM huku alibainisha kuwa katika nafasi hakukuwa na upinzani wa chama kingine kwani chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakikuleta mgombea japo kuwa wana diwani Moja kutoka katika chama hicho.



Aidha aliwapongeza madiwani wote kwa kufanya uchaguzi wa kumchagua naibu meya kwa utulivu na amani huku akiwaasa kuondoa kasoro ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kwa muda mrefu kwa kutokufanya kazi kwabidii na badala yake katika mwaka huu wa fedha 2022/2023 wajitaidi zaidi kuealetea maendeleo ya wananchi wao



Alisema wameanza mwaka mwingine wa utekelezaji ilani ya chama halmashauri yao imepitia katika kipindi ambacho ilipata kashfa ya ubadhilifu wa fedha na kunabaadhi ya watu walishachukuliwa hatua za kisheria ambapo alibainisha umefika wakati wa kila mmoja kujitafakari na kuwaza kufanya kazi kwa bidii Ili kuweza kutatua matatizo ya wananchi 


Alisema kuwa Kwa mwaka 2022/2023 Jiji la Arusha wamejipanga ipasavyo kuhakikisha mapato ya halmashauri yanapanda pia miradi yote waliyo iazisha inatimia kwa wakati ili kuwezesha wananchi kupata huduma aidha pia wameweka mikakati mizuri ya kuweka miradi ya utalii ili watalii wanapofika katika jiji hili wasiwe wanapitiliza hifadhini moja kwa moja ila watulie sehemu nzuri ili kuweza kuipatia fedha za kigeni halmashauri 


 Akizungumza mara baada ya kupitishwa naibu Meya Veronica Mwelange aliwataka madiwani hao kuwa wapya kama ilivyo mwaka mpya wa fedha huku akiwataka kuunganisha nguvu kujenga halmashauri hiyo.


Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo aliwataka madiwani hao kufanya kazi kwa umoja na kwabidii ambapo aliongeza kuwa pia ni wajibu wao kama viongozi wa halmashauri kufatilia na kujirizisha na mwenendo ambao halmashauri unakwenda nao.



"Tunafahamu kuna kiasi cha fedha kingi kimepotea ,watu wamechukuliwa hatua za kisheria lakini hiyo aitunyimi sisi kama madiwani kuendelea kufahamu nini kimetokea ,fedha zimetumikaje,zimeenda wapi na sisi kama madiwani tuchukuwe hatua zetu kama madiwani Ili mambo hayo yasiweze kujirudia"alibainisha Gambo.


Alisema kuwa wanapokwenda kuanza mwaka mpya wa fedha wakae chini wajipange ,waangalie nini kipaumbele chao waangalie jambo gani wakifanya kitawasaidia katika kipindi cha uchaguzi unaofata  


Aliwataka waendelee kuweka mbele maslahi ya wananchi kwani wananchi wa jimbo la Arusha wanajielewa sana na kujitambua hivyo ili kazi yao iweze kuwa nzuri ni vyema wakaweka mbele maslahi ya wananchi ,pamoja na kuangalia changamoto zilizopo ,waziongelee kwenye vikao vyao na wasikubali kuburuzwa, wasome kanuni vizuri pamoja na sheria Ili waweze kuwawakilisha wananchi wao vyema na kusaidia kutatua kero zao.


Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates