BREAKING NEWS

Wednesday, July 13, 2022

CWT WATAKA KIKOKOTOO KURUDI KWA WADAU ILI KIJADILIWE UPYA



Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na umoja wa viongozi wa chama cha walimu Tanzania Kanda ya nyanda za juu kusini (SOHITCO) inaindwa na Mikoa sita ambayo ni Iringa, Mbeya, Njombe,Songwe,Rukwa,na Katavi wakati wa mkutano mkuu wa umoja huo ulifanyika mkoani Iringa
Mwenyekiti wa chama cha walimu mkoa wa Iringa Stanslaus Mhongole akiongea na umoja wa viongozi wa chama cha walimu Tanzania Kanda ya nyanda za juu kusini (SOHITCO) inaindwa na Mikoa sita ambayo ni Iringa, Mbeya, Njombe,Songwe,Rukwa,na Katavi wakati wa mkutano mkuu wa umoja huo ulifanyika mkoani IringaBaadhi ya walimu viongozi wakiwa kwenye mkutano mkuu wa umoja wa viongozi wa chama cha walimu Tanzania Kanda ya nyanda za juu kusini (SOHITCO) inaindwa na Mikoa sita ambayo ni Iringa, Mbeya, Njombe,Songwe,Rukwa,na Katavi uliofanyika mkoani IringaBaadhi ya walimu viongozi wakiwa kwenye mkutano mkuu wa umoja wa viongozi wa chama cha walimu Tanzania Kanda ya nyanda za juu kusini (SOHITCO) inaindwa na Mikoa sita ambayo ni Iringa, Mbeya, Njombe,Songwe,Rukwa,na Katavi uliofanyika mkoani IringaBaadhi ya walimu viongozi wakiwa kwenye mkutano mkuu wa umoja wa viongozi wa chama cha walimu Tanzania Kanda ya nyanda za juu kusini (SOHITCO) inaindwa na Mikoa sita ambayo ni Iringa, Mbeya, Njombe,Songwe,Rukwa,na Katavi uliofanyika mkoani Iringa



Na Fredy Mgunda,Iringa.

 

CHAMA cha walimu Tanzania (CWT) imeitaka serikali kukirudisha kikokotoo kilichopendekezwa kwa wadau ili kijadiliwe kwa kuwa sasa kinawaumiza wafanyakazi pale wanapoenda kustaafu.

 

Akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa umoja wa viongozi wa chama cha walimu Tanzania Kanda ya nyanda za juu kusini (SOHITCO) inaindwa na Mikoa sita ambayo ni Iringa, Mbeya, Njombe,Songwe,Rukwa,na Katavi,Katibu wa chama cha walimu mkoa wa Iringa (CWT),Hamisi Chinahova alisema kuwa walimu wamekuwa wakifanya kazi kwa kujitolea muda wote kwa kulijenga taifa hili.

 

Chinahova alisema kuwa walimu wamekuwa wanafanya kazi kwa weledi mkubwa kuhakikisha wanawafundisha Wanafunzi kwa juhudi kubwa hivyo serikali inatakiwa kukiangalia upya kikokotoo hicho.

 

Alisema kuwa walimu wanakumbana na mazingira duni ya kufanyia kazi ikiwapo pamoja upungufu wa vifaa vya kufundishia 

 

Chinahova alisema kuwa walimu wamekuwa wanadai madeni mbalimbali na ya muda mrefu hivyo wanaiomba serikali kuhakikisha wanatatua changamoto ya madai ya walimu ili waendelee kufanya kazi wito kama awali.

 

 

Alisema kuwa watumishi walimu wasipangiwe bank ya kutumia kupitisha mishahara yao kwa kuwa hiyo ni haki ya msingi na serikali inapaswa kuridhia swala hilo.

 

Chinahova alimazia kwa kusema kuwa serikali inatakiwa kuendelea kuajiri walimu wengi sambamba na ujenzi wa madarasa ili kuwapunguzia changamoto walimu wakiwa kazini.

 

Kwa upande wake mgeni rasmi katika mkutano huo,mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa chama cha walimu Tanzania kinafanya kazi kubwa ya kuishauri serikali juu ya upatikanaji wa ajira za walimu ili kuongeza ufanisi katika sekta ya elimu.

 

 

Moyo alisema kuwa walimu wamekuwa chachu ya mabadiliko ya muundo wa serikali juu ya watumishi ili kuhakikisha watumishi wanapata haki zao za msingi.

 

 

Alisema kuwa serikali ya mkoa wa Iringa italifanyia kazi haraka swala la kuwarudisha wastaafu mapema makwao mara baada ya kustaafu kwa kuwa wamelitumikia taifa hili kwa miaka yao yote ya utumishi ambapo wamechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Tanzania.

 

Moyo alisema kuwa serikali inaendelea kutatua changamoto ya miundombinu ya shule na vifaa vya kufundishia na kujifunzia kadri fedha inavyopatikana.

 

Alimazia kwa kusema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imeanza kufanya maboresho kwenye sekta ya elimu na kuonyesha nia yake ya kuendelea kuboresha sekta hiyo.

 

 

Nao baadhi ya wenyeviti wa CWT nyanda za juu kusini walisema kuwa kufanya kazi kwa ushirikiano ndio jambo ambalo litasaidia taasisi hiyo kukua kila wakati.

 

Walisema kuwa mshikamano kazini ndio kitu bora kwa wafanyakazi walimu kuendelea kutunza nidhamu kazi kwa kuwalea watoto katika maadili yanayotakiwa.

 

 

 Walisema kuwa walimu ndio wamekuwa chanzo cha maendeleo ya nchi ya Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kuwa viongozi bora kwenye sekta mbalimbali.

 

 

Waliongeza kwa kusema kuwa walimu ni wito jambo ambalo limekuwa kukisaidia kuzalisha wasomi wengi wenye tija ya kimaendeleo.

 

Walisema kuwa walimu wanapaswakutimiza wajibu wao kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria zote za kazi na nini katiba ya nchi inavyosema.

 

 

Lakini pia mkuu wa wilaya ya Momba Faki Lulandala aliwataka viongozi wa CWT kutetea maslai ya wafanyakazi walimu ili kuendeleza umoja na maslai ya walimu.

 

Lulandala alisema chama cha walimu ndio chama kikubwa kuliko vyama vyote vya wafanyakazi Africa kutokana na umoja na mshikamano uliopo licha ya mara kadhaa kukumbana na changamoto mbalimbali.

 

Alisema kuwa utulivu na mshikamano uliopo hapa nchini unatokana uongozi wa CWT kuwa umoja na utulivu uliopo hivyo viongozi wanapaswa kuendelea kudumisha utamadumi uliopo toka zamani.

 

 

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates