Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amewataka vijana wa Tanzania kuwa wazalendo pamoja kuifia nchi yao Ili kuendelea kulinda na kuenzi amani ya nchi yetu
Aliyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa Mkoa na baadhi ya wananchi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya mashujaa ambapo kwa Mkoani wa Arusha imefanyika katika bustani ya mashujaa iliopo ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha
Alisema kuwa kumbukumbu ya mashujaa walioipigania nchi ni fundisho kwa watanzania kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano ili nchi yetu iwezo kusonga mbele.
Alibainisha kuwa mashujaa hao waliweza kuipigania nchi ndio maana hadi leo nchi yetu ina amani na utulivu mwingi.
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akibadilishana mawazo na Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Pindi Chana mara baada ya zoezi la uwekaji wa silaha za jadi ikiwemo ngao,mkuki,shoka na sime katika sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa yaliyofanyika leo ambapo kwa mkoa wa Arusha yamefanyikia katika bustani ya Mnara wa Mashujaa iliopo ndani ya halmashauri ya Jijini Arusha na kuuthuriwa na baadhi ya Mavetenari waliopigana Vita vya Kagera
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia