BREAKING NEWS

Tuesday, July 19, 2022

35 KUSHIRIKI AFRICAN RALLY CHAMPION ROUND 4

 

mratibu wa mashindano ya magari Afrika (Afrika Rally champion ship )kwa mwaka 2022 Satinder Birdie  wa pili kulia akiongea na waandishi wa habari juu ya mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi July 22 hadi 24 wilayani monduli mkoani ARUSHA
Wa kwanza kushoto mwakilishi wa kampuni ya Atlantic Lubricants ,Sharan Aggarwal akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wathamini wa mashindano hayo




Na Woinde Shizza , ARUSHA 

TANZANIA ATLANTIC RALLY 2022
Mzunguko wa Nne 4) wa Mashindano ya Magari ya Afrika unaofahamika kama Africa Rally Champion Ship Mwaka 2022 unatarajiwa  kuanzia July 22 hadi 24 mwaka huu katika eneo la Monduli Mkoani Arusha ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa Mashindano hayo kufanyika Nje ya Mkoa wa Pwani.

Klabu ya Mbio za magari Arusha kwa kushirikiana na chama kinachosimamia Mashindano ya mbio za magari Tanzania (AAT) kwa pamoja watafanya Mashindano hayo yanayofahamika kwa jina la  Tanzania Atlantic Rally ambayo yanajumuisha na ligi ya ndani ya mbio za Magari mzunguko wa Tatu

Mratibu wa Mashindano hayo Satinder Birdi kando na kuwashukuru wadhamini ameelezea umuhimu wa Mashindano hayo  ni pamoja na  kuhamasisha maendeleo ya Mchezo wa Mbio za Magari

Aidha alisema kuwa jumla ya madereva  35 watashiriki  katika mashindano hayo kati yao 13 wanatoka katika  nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo saba kutoka Kenya Moja kutoka Zambia ,mmoja kutoka Rwanda ,wawili kutoka nchini Uganda  na huku wengine wote waliobaki wakitokea nchini Tanzania 

"Kitu kinachofurahisha zaidi katika mashindano ya mwaka huu tunakivutio cha kipekee ambacho bila shaka mashabiki wengi watafurahia  kwani mashindano haya yamebahatika kumpata  mshiriki mmoja mwanamke ajulikanaye kwa jina la Maxin Wahome  ,tunaamini atakuwa kivutio sana kwa mashabiki"alisema


Akizungumza kwa niaba ya wadhamini,mwakilishi wa Kampuni ya Atlantic Lubricants Sharan Aggarwal aliwataka  wadhamini zaidi wajitokeze ili kukuza  mchezo huo ambao unaonekana kuimarika kwa kasi,huku akibainisha kuwa mashindano hayo yataazia  katika viunga vya hoteli ya Mount Meru Arusha na kuelekea wilayani Monduli 


 Kwa upande wake meneja wa hoteli hiyo Jonathan Cox ametoa  wito kwa washiriki na Mashabiki kujitokeza kwa wingi kushiriki na kujionea mashindano hayo.


Naye Afisa Usalama wa Mashindano hayo Goodluck Mariki aliwataka washabiki pamoja na madereva   kuchukuwa  tahadhari zote za kiusalama pindi wanapo kuwa katika  mashindano hayo ikiwa ni pamoja na kufuata sheria na maagizo yote wanayopewa na watu wa usalama 

Aidha alitaja baadhi ya magari ambayo yatakuwepo katika mashindano haya kuwa ni Ford fiesta Rs, Mitsubishi Lancer Evo x,,Subaru Impreza, Skoda proto pamoja na Hyundai 120 R5 ambayo  ndio gari pekee ambayo inaingia katika mashindano haya kwa mara ya kwanza.

Alibainisha kuwa mashindano ya ni ya mbio za magari ya Afrika  ambayo nia yake ni kumtafuta  dereva mmoja ambaye ataongoza kwa ushindi kwa nchi za Afrika  na hii ni raundi ya nne tangu kuanza kufanyika ,hadi  yalishafanyika katika nchi ya Kenya ,Zambia ,Ivory coast  na raundi hii ya nne inafanyika nchini Tanzania  mkoani Arusha



Katika Msimu huu Mashindano hayo yanategemewa kuwa na ushindani Mkubwa kutoka kwa madereva wa ARC pamoja na wale wa NRC  kila upande madereva nguli  kushinda  Rally moja moja katika mizunguko yote.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates