Mkuu wa wilaya ya karatu Dadi Kolimba akiongea sherehe za maathimisho ya zoezi la mashindano ya uandishi wa insha kwa kupinga mimba na ndoa za utotoni ngazi ya mkoa
Na Woinde Shizza ARUSHA
Alisema lengo kuu la shindano hilo ni kupinga mimba na ndoa za utotoni ambazo huathiri safari ya masomo kwa watoto wa kike na kushindwa kufikia ndoto zao katika maisha.
Alisema mwaka 2022 kwa Mkoa wa Arusha watoto waliofanyiwa ukatili wa kijinsia 4356 ambapo alifafanua kwa halmashauri ya jiji la Arusha ndio linaongoza kwa vitendo hivyo ambapo jumla ya matukio 2140 ya ukatili yamefanyika ambapo kati yao matukio ya ukatili wa kingono yakiwa 774.
Alisema halmashauri iliofata ni ya Meru ambapo kulikuwepo na jumla ya matukio 721 ya ukatili wa kijinsia ambapo kati yake matukio ya ubakaji na ulawiti yakiwa 95,katika halmashauri ya Arusha DC matukio ya ukatili yalikuwa 651 kati ya hayo matukio matukio ya ubakaji na ulawiti ni 134,wilaya ya karatu matukio ya ukatili yalikuwa 365 kati yake matukio ya ulawiti na ubakaji ni 102,wilaya ya Longido matukio ya ukatili yalikuwa 98 kati yake matukio saba yalikuwa ya ukatili wa kingono katika halmashauri ya Monduli matukio ya ukatili wa kingono yalikuwa 209 ambapo kati yake matukio ya ukatili wa kingono yakiwa 14
Akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela mkuu wa wilaya ya karatu Dadi Kolimba alisema kuwa Shindano hili la insha litasaidia kuwajenga watoto wa kike kutokudanganyika kuingia katika mitego ya kupata mimba pamoja na ndoa za utotoni kwa ajili ya ustawi wa mkoa na Taifa kwa ujumla
Alisema kuwa ili kupambana na tatizo hilo serikali ya Mkoa imekuwa ikiendelea na jitihada mbalimbali za kupambana kupunguza au kumaliza kabisa tatizo hilo kwa kukaa vikao na wadau mbalimbali wa elimu,waalimu,wazazi pamoja na wanafunzi wenyewe.
Kwa upande wake meneja wa shirika la Word vision mkoani Babati Gloria Mashingia alisema kuwa jumla ya wanafunzi 5000 wameshiriki shindano hilo
la uandishi wa insha kutoka katika shule 47 za mkoa wa Arusha.
Alisema kuwa katika shindano hilo washindi katika kumekuwa na washindi kutoka ngazi ya Wilaya,Mkoa pamoja na Kitaifa ambapo alifafanua kuwa wote walioshinda katika ngazi ya mkoa wataenda kushiriki katika mashindano hayo ngazi ya Taifa
Alisema kuwa katika mashindano haya washindi wote waliondoka na baiskeli pamoja na kitita cha fedha taslimui ambapo pia ali wataka walimu kama walezi wakuu wa vijana kuendelea kuwapa wanafunzi elimu
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia