Akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kutangaza Uzinduzi wa mbio hizo, Mkurugenzi wa taasisi ya michezo ya Meta, ambao ndio waandaji, Meta Petro alisema wamefungua fursa ya usajili ili kutoa nafasi kwa wanariadha kuanza kujiwekea nafasi ya ushiriki katika mbio hizo za kimataifa.
Alisema kuwa wanatarajia wanariadha zaidi ya 2000 kushiriki katika mashindano hayo, kutoka nchi mbali mbali ikiwemo za Kenya, Uganda na Rwanda na wenyeji Tanzania bara na visiwani ambao wamekuwa wakisumbua kutaka kujua mbio zinafanyika lini huku wakionyesha Nia ya kushiriki.
"Kama unavyojua mbio zetu huwa tunafanya mwezi April lakini kutokana na baadhi ya changamoto zilizokuwa nje ya uwezo wetu tuliamua kuhairisha Hadi mwezi September lakini kipindi hicho chote wako wanariadha hasa wa nje ambao hawakuweza kupata taarifa za kuhairisha kwetu, hivyo rasmi sasa tunawaalika waje kushiriki mbio hizi ambazo zimekuwa za kihistoria nchini Tanzania na viunga vyake.
Meta
alisema kuwa katika mbio hizo ambazo zinalenga kutangaza utalii wa
Tanzania kwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania mama
Samia Suluhu Hassan, wameandaa zawadi mbali mbali kwa waashiriki wote
na washindi ikiwemo medali, t-shirt na fedha taslim kwa washindi wa
kwanza 15.
Alisema gharama ya usajili katika mbio hizo ni 35,000, tu ambayo italipwa na mshiriki na kuchagua umbali atakaopenda kukimbia.
Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni ya market access, George Damian alisema kuwa wameamua kudhamini mashindano hayo ili kuyaongezea thamani.
Nae katibu wa chama Cha riadha mkoa wa Arusha, Rogath Steven alisema kuwa wameungana na waandaaji wa mbio hizo ili kufanikisha kuvuna wanariadha wenye vipaji ambao watasaidia mkoa na nchi kwa ujumla kuwa na akiba na vipaji.
"Mashindano haya yamekuwa na faida kubwa kwetu, kwani yanatukutanisha na vipaji vipya kila Mara za wanariadha ambao tumekuwa tukiwatumia katika kukuza na kuwaonyesha fursa ya kuwaendeleza lakini pia kupata wanariadha wapya watakaotuwakilisha kitaifa na kimataifa"
Rogath alitumia nafasi hiyo, kuwaalika wanariadha wote kushiriki mashindano hayo, pia vijana chipukizi wanaotaka kuonyesha vipaji vyao kutoka maeneo mbali mbali nchini.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia