BREAKING NEWS

Wednesday, July 6, 2022

WAFAMASIA ZAIDI YA 20 KUTOKA MIKOA SITA YA TANZANIA BARA WAPATIWA MAFUNZO MAALU ARUSHA




 Zaidi ya Wafamasia 28 toka Mikoa 6 ya Tanzania Bara wanapatiwa Mafunzo Maalum kuhusu Mifumo ya Ufuatiliaji wa Usalama wa Dawa,Vifaa Tiba pamoja na Chanjo yanayofanyika Jiji Arusha.


Akizungumza katika ufunguzi wa Warsha hiyo,Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt Athumani Kihamia ambaye alikuwa Mgeni rasmi amesema kuwa Mafunzo hayo ya Siku mbili ni muhimu sana kwa Kada ya Wafamasia Nchini Tanzania kwani yatawajengea uwezo wa kukabiliana na athari hasi zinatokea katika matumizi ya dawa,Chanjo na Vifaa tiba vinavyotolewa kwa Wagonjwa hii itasaidia Wanajamii kupata taarifa sahihi ili kuepusha sintofahamu kutokana na madhara.


"Ni seme tu pamoja na faida tunazopata za kimatibabu kupitia dawa,vifaa tiba pamoja na chanjo mara chache kumekuwa kukitokea madhara kwa watumiaji,hivyo kupitia mafunzo haya nitoe rai kwa Wafamasia kutoa taarifa sahihi za usalama wake kwa Jamii ili kuzuia athari kwa Wagonjwa wengine." Alisema Dkt.Kihamia.


Sambamba na hilo,Dkt.Kihamia amewataka Wakufunzi na Wafamasia hao kutumia njia shirikishi katika Mafunzo hayo ili kuleta uelewa wa pamoja kwa kutumia uzoefu kutoka maeneo yao ya kazi kuhusu hali ya usalama wa dawa vifaa tiba pamoja na chanjo kwa lengo kuisaidia Serikali katika kukabiliana na changamoto za athari hasi za matumizi ya dawa hizo ili kulipungumzia Taifa mzigo kwa kupeleka Wagonjwa nje ya Nchi kwa matibabu baada ya kupata athari kutoka na matumizi ya dawa,vifaa tiba pamoja na chanjo.


Mafunzo hayo ya Siku mbili yanafanyika Chuo cha CEDHA Arusha kwa kujumuisha Wafamasia wa Mikoa ya Arusha, Manyara,Kilimanjaro, Tanga,Dodoma na Singida.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates