BREAKING NEWS

Tuesday, July 12, 2022

WANANCHI WA JIJI LA ARUSHA WAONGOZA KWA KUTUPA TAKA NGUMU KATIKA VYANZO VYA MAJI




 Na Woinde Shizza , ARUSHA


Wananchi wa halmashauri ya jiji la Arusha wanaongoza kwa kitendo cha kutupa taka ngumu katika vyanzo vya maji huku baadhi ya wengine wakiwa wamejenga karibu na vyanzo hivyo vya maji



Akiongea na waandishi wa habari ofisa maendeleo jamii mkuu kutoka bonde la maji bodi ya pangani Jane Kabogo mara baada kutoa elimu kwa wadau ,madiwani ,watendaji wa mitaa watendaji wa kata pamoja na wenyeviti wa mitaa na wananchi wanaoishi pembezoni mwa vyanzo vyama maji kutoka katika mito ya Ngarenaro ,Themi na kijenge iliopo ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha lengo haswa likiwa kuwashirikisha katika zoezi linaloendelea la uwekaji wa mipaka katika vyanzo vya maji pamoja na kutimiza kauli mbiu ya bonde la pangani ambayo inasema utunzaji wa vyanzo vya maji nijukumu letu sote kwaiyo Kila mmoja anajukumu la kutunza vyanzo vya maji


Alisema kuwa suala la utupaji taka katika vyanzo vya maji limekithiri katika halmashauri ya jiji la Arusha huku baadhi ya wananchi wakiwa wanakiuka sheria na kujenga karibu na vyanzo vya maji pamoja na kufanya shuguli za kibinadamu kwenye vyanzo hivyo jambo ambalo nikinyume na sheria za bonde la pangani


Alisema kutokana na tatizo hilo ndio maana wameweza kuwakutanisha wadau hawo ili kuweza kuwapa elimu ya madhara ya kutupa taka katika vyanzo vya maji pamoja na madhara ya kujenga karibu na vyanzo hivyo.


Alibainisha ni vyema kila mtu kwa nafasi yake kutunza mazingira hususa vyanzo vya maji kwa sababu sio bonde la pangani tu wamekaimishwa kusimamia vyanzo hivyo bali hata wananchi wanawajibu wa kutunza kwa nafasi yake kwani maji hayo yanayopatikana yanawasaidia pia.



Kwa upande wake afisa mazingira kutoka bonde la pangani Felister Joseph alisema kuwa pamoja na hayo lengo lingine la kuwakutanisha wadau hawa ni pamoja na kuwapa elimu pamoja na kuwashirikisha wananchi kuhusu uwekaji wa alama za mipaka na utunzaji wa alama hizo ambapo pia alisema kuwa wameweza kuwaeliza wananchi kwanini alama hizo zinapaswa kulindwa na walinzi wakubwa ni wao wenyewe.


"Niwaombe wananchi waweze kutoa ushirikiano maafisa wa bonde la pangani wanapoenda kuweka alama hizo pia tunaomba sana waendelee kutunza vyanzo hivyo vya maji vilivyopo katika maeneo yao"alisema Felister 


Alisema kuwa wanapo linda na kutunza vyanzo hivyo vya maji vinawasaidia wao wenyewe kwa matumizi ya sasa na hata baadae kwa vizazi vijavyo.


Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates