BREAKING NEWS

Wednesday, July 6, 2022

MKOA WA ARUSHA WAVUKA LENGO LA UANDIKISHAJI WATOTO CHINI YA MIKA 5




 Mkoa wa Arusha wavuka lengo la Kitaifa katika zoezi la Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto wenye umri chini ya miaka mitano ambalo lilianza Mwaka Juni,2021.


Akizungumza katika Kikao hicho cha Tasmini,Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema Mkoa umevuka lengo la Kitaifa la Usajili na Utoaji Vyeti kwa watoto chini ya miaka mitano baada ya kuweka mikakati madhubuti ya uhamasishaji na ufuatiliaji kuanzia ngazi za Vituo vya Afya kwa mama anapojifungua kupewa cheti rasmi cha mtoto hivyo kupelekea zoezi kufanyika kwa umakini na kuuwezesha Mkoa wa Arusha kufikia 80.2% ya lengo la Kitaifa lililotaka kufika 80% kwa kipindi cha mwaka mmoja toka lizinduliwe mwaka 2021.


"Napenda saana kutoa pongezi kwa Watendaji wote wa Kada ya Afya hususani watoa huduma za Mama na Mtoto kwa jitihada kubwa ya kusajili watoto chini ya miaka mitano hii imetuletea heshima kwa Mkoa wetu wa Arusha." Alisema Mongella


Mhe.Mongella amesema pamoja na mafanikio hayo ya kuvuka lengo la Kitaifa kwa Mkoa wa Arusha bado amewataka Viongozi na Watendaji wa Kada ya Afya kwa pamoja kushirikiana ili kuweza kufikia kengo la uandikishwaji na usajili wa vyeti kwa asilimia 100 ifikapo Mwezi disemba,2022.


"Nawaagiza Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri kwa kushirikiana Waganga Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia zoezi hili kwa kutenga fedha ili kuunga na wadau wetu wa UNICEF." Alisema Mongella


Kwa upande wake Naibu Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali Mkoa wa Arusha Bi.Lina ameipongeza Timu ya Watalaam na Halmashauri zote kwa namna walivyoweza kufanya kazi kwa kushirikiana na RITA na UNICEF na kufanikisha zoezi la uandikishaji watoto chini miaka mitano.


Kikao hicho cha siku moja kilihudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala,Wakurugenzi wa Halmashauri,Wenyeviti wa Halmashauri ,Mganga Mkuu wa Mkoa,Waganga wa Wakuu wa Wilaya, Waratibu za zoezi la Usajili ambao ni Maafisa Ustwi wa Jamii,Viongozi wa Dini pamoja na Waratibu wa Huduma za Uzazi na Mtoto.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates