BREAKING NEWS

Tuesday, July 5, 2022

KISWAHILI CHAZIDI KUITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA



Shamimu Nyaki, Dar es Salaam 


Kiswahili imechangia kuitangaza Tanzania kutokana na lugha hiyo kuwa miongoni mwa lugha zenye wazungumzaji wengi ulimwenguni. 


Akizungumza katika siku ya Maandamano ya hiari ya kuelekea Siku ya Kiswahili Duniani, Julai 03, 2022 Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Bi. Consolata Mushi amesema lugha hiyo imepata heshima kubwa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kuitengea siku yake maalum ya kuadhimishwa ambayo ni Julai 07 ya kila Mwaka.

 "Maadhimisho haya ni kudumisha heshima tuliyopewa na UNESCO kama watumiaji wa lugha hiyo, na tutaitumia fursa hii kukuza na kuendeleza lugha yetu adhimu kwa vizazi vyote" amesema Bi. Consolata.



Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates