Chama cha walimu Mkoa wa
Arusha(CWT)kimeitaka serikali kuhakikisha inaboresha maslahi bora ya
walimu ikiwemo mazingira mazuri ya kufundishia na kulipa stahiki za
walimu kwa wakati pindi wanapohamishwa vituo vya kazi.
Akiongea
na waandishi wa habari katika kikao kazi cha wafanya maamuzi ngazi ya
halmashauri na Mkoa,mwenyekiti wa CWT mkoani hapa,Mwl.Lotta Laizer
alisema kuwa pamoja na Rais Samia Sululu Hasani kujitahidi kutatua
baadhi ya changamoto ikiwemo nyongeza ya mshahara lakini bado hangamoto
ni kubwa.
Laizer
alisema kuwa serikali kama mwajiri wa walimu nchini inawajibu wa
kuhakikisha walimu wanapata stahiki zao sahihi kwa wakati jambo litakalo
saidia kuongeza morari wa kufundisha na kuongeza ufaulu nchini.
"Kuna
changamota nyingi ambazo kimsingi mwalimu anastahili kuzipata
ikiwemo,mfumo wa taarifa ,mabadiliko ya zama,kucheleweshwa kwa stahiki
za walimu ,sheria kandamizi za kazi "alisema .
Hata
hivyo alimpongeza Rais Samia kwa kuwaongezea mishahara walimu na
kupunguza baadhi ya changamoto zilizokuwa zikiwakabili kwa muda mrefu.
Katibu
wa CWT,Abraham Kamwela,alisema kikao hicho kiliwashirikisha viongozi
wa CWT Mkoa na wilaya ,wafanya maamuzi wakiwemo wakurugenzi wa
halmashauri wakuu wa wilaya na makatibu wakuu wa wilaya ,maafisa elimu
na utumishi lengo likiwa ni kufahamishana mabadiliko mbalimbali ya
sheria.
"Kwa mfano sheria
ya ajira na Mahusiano kazini inayo mabadiliko kadhaa inayohusiana na
uendeshaji wa vyama vya wafanyakazi,hivyo tukikaa pamoja tunaweza
kutafisiri mabadiliko hayo na kuondoka na Jambo moja"alisema.
Naye
kaimu afisa elimu Mkoa wa Arusha,Shelley Swai alisema mkoa wa Arusha
unachangamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa walimu wa shule za
msingi na serikali.
Alisema mkoa wa Arusha unauhitaji wa walimu 8573 na waliopo ni 6738 tu,hivyo upungufu ni walimu 1793 .
Awali
kaimu katibu tawala mkoa wa Arusha David Lyamongi alisema mkoa wa
Arusha umekuwa ukifanya vizuri kwa matokeo mazuri ya ufaulu kutokana na
jitihada zinazofanywa na wadau wa elimu
Lyamongi
aliwasisitiza CWT kuweka mazingira mazuri na mahusiano baina ya
serikali na chama Cha walimu ili kuondoa mivutano kati ya mwajiri na
chama hicho hasa kuhusu suala la masilahi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia