BREAKING NEWS

Wednesday, July 20, 2022

WAKUU WA NCHI SABA ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUKUTANA ARUSHA



 Wakuu wa nchi 7 kutoka jumuiya ya Afrika Mashariki wanatarajia kukutana Jiji Arusha Kwa lengo kujadili jinsi ya kuinua uchumi wa wananchi wa jumiuiya ya Afrika mashariki ikiwa ni kikao cha kawaida cha wakuu hao.


Akiongea na waandishi wahabari Jiji Arusha katibu mkuu wa jumuiya hiyo Peter Mathuki amesema baada ya uviko 19 kwa vikao vya wakuu hao kufanyika kwa njia ya mtandao Sasa wakuu hao wanakutana katika kikao cha 22 kawaida cha wakuu hao kwenye makao makuu ya jumuiya hiyo 


Amesema lengo la mkutano huo ni kuona namna ya kukuza uchumi katika biashara za maingiliano katika mipaka na suala Zima la kukuza mtangamano Kwa wananchi wa mataifa hayo yanayokadiriwa kuwa na watu milion 200 kwa sasa .


Kwa Mujibu wa Dkt. Mathuki katika Mkutano huo nchi ya Jamhuri ya watu wa Kongo (DRC) itashiriki mkutano huo ikiwa ni mara ya kwanza kushiriki tokea ijiunge na umoja huo. 


Amesema kuanguka Kwa uchumi wa jumiuiya kutokana na changmoto uviko 19 kikao hicho cha wakuu wa jumuiya ya Afrika mashariki kimelenga kujenga suala Zima mtangamano kujadili ushuru wa forodha na changamoto zinazoikabili jumuiya hiyo .



Marais 7 wanatarajiwa kushiriki Mkutano huo wakiongozwa na Mwenyeji wao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye anatarajiwa kuwasili Mkoani Arusha Leo tarehe 20 Julai 2022


 "Wakuu wanakutana kwa siku mbili ikiwa ni Kikao cha kawaida kujadili changamoto mbalimbali zilizoikumba nchi za Jumuiya na kama mnavyokumbuka DRC itashiriki kwa mara ya kwanza hivyo wakuu wote wa nchi zetu watashiriki Mkutano huo na pia kuzindua barabara ya Afrika Mashariki ya Bypass"


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela amesema kuwa maandalizi ya mkutano huo wa Wakuu wa nchi yamekamilika ambapo kesho wanatarajia kumpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu na baadae Marais sita wa jumuiya ya Afrika mashariki.ambapo tarehe 21 wanatarajia kuzindua Barabara ya Afrika mashariki (by pass)


Amesema kuwa baada ya uzinduzi wa barabara hiyo viongozi hao watakutana katika kikao chao cha kawaida ambapo amewataka wakazi wa mkoa wa Arusha kujiandaa na ugeni huo Kwani mkoa umepewa heshima kubwa na nchi Kwa ujumla ya kuwa waandaaji wa mkutano huo.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates