BREAKING NEWS

Monday, July 25, 2022

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAJIPANGA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA SEKTA YA UTALII

 

Waziri wa maliasili na utalii Balozi dkt Pindi Chana akiongea katika mkutano wa wadau wa sekta ya utalii (MPPD)leo mkoani Arusha.





Na Woinde Shizza , ARUSHA 

SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imejipanga 
kushirikiana na wadau wa sekta binafsi kujadili mapendekezo ya sera
sheria taratibu na kanuni kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara
na uwekezaji nchini ikiwemo biashara ya Utalii ambapo imedhamiria
kuboresha mazingira ya biashara hiyo.

Aidha  Serikali imejipanga kuhakikisha inatengeneza mfumo wa
pamoja wa biashara baina ya wadau wa Utalii ikiwa ni lengo la kupata
huduma zote sehemu moja za tozo kodi na malipo yote ya sekta hiyo(One
stop Shop) ili sekta hiyo ichangie kikamilifu katika uchumi

Akiongea wakati akifungua mkutano wa Wadau wa sekta ya Utalii (MPPD)
Jijini Arusha Waziri wa Maliasili na Utalii balozi Dkt, Pindi Chana amesema kwamba maagizo aliyotoa Mh.Rais Samia Suluhu Hassan kwenye
Mkutano wa 13 wa baraza la taifa la biashara TNBC jijini Dodoma
alituagiza tukutane na sekta binafsi hususani sekta ya Utalii kujadili
mapendekezo na mageuzi ya sera sheria kwa lengo la kuboresha mazingira
ya biashara hiyo.

Amesema kwamba serikali imedhamiria kwa dhati kuboresha mazingira ya
biashara na uwekezaji katika sekta ya Utalii ili ichangie kikamilifu
katika uchumi na maendeleo ya Taifa letu kwa ujumla pia dhamira hii
inaenda sambamba na uendelezaji wa malengo a kimkakati ya mpango wa
Tanzania The Royal Tour katika kukuza Utalii kadhalika na Uhifadhi wa
maliasili na malikale zetu.

Awali akiongea wakati akimkaribisha Waziri Chana katika kikao hicho
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Eliaman Sedoyeka
alisema kwamba kupitia wizara hiyo wamejipanga kuongeza juhudi kubwa
za kuutangaza Utalii duniani ikiwa ni ishara ya kuunga juhudi za Rais
Samia Suluhu Hassan alieafanya kwa vitendo kuandaa Filamu ya Royal
Tour.


Amesema Pamoja na sekta hiyo kuathiriwa na uwepo wa janga la Uviko 19
sanjari na vita baina ya mataifa ya Urusi na Ukrein bado wizara
itaendelea kupanua soko la utalii kufikia malengo ya watalii milion 5
mwaka 2025.

Kwa Upande wake Mshauri wa Mazingira ya Uwekezaji IFC Anita Kundy
amesema kwamba Tangu 1956, IFC imewekeza zaidi ya dola bilioni 2.8
katika miradi zaidi ya 260 katika nchi 89 na zaidi ya nusu ya
uwekezaji huu katika nchi nyingine. Nchini Tanzania, tumewekeza pia
katika hoteli jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Dunia na Baraza la Utalii, kila dola inayotumika kwa
usafiri na utalii inazalisha zaidi ya dola tatu za pato la kiuchumi.

Zaidi ya wafanyakazi milioni 100 wameajiriwa katika sekta hii duniani
kote, na mapato ya utalii yanachangia mtiririko wa fedha zaidi kwa
nchi zinazoendelea kuliko mtiririko wote wa misaada kutoka kwa
wafadhili wa kigeni.

 Alisema IFC inafuraha kuunga mkono na kusapoti kufikiwa kwa malengo
muhimu ya serikali ya awamu ya 6 ya kuifanya Tanzania kama kivutio cha
utalii na uwekezaji. Kwa miaka sitini, IFC, mwanachama wa Benki ya
Dunia, imefanyakazi na sekta binafsi kwenye kuleta masuluhisho
yaliyoleta mabadiliko chanya kijamii na kiuchumi.




Kwa Mujibu wa Kundy amesema imefanikisha hili kwa kuunda masoko mapya,kuhamasisha wawekezaji binafsi, na kutoa msaada wa kitaalamu ,IFC inawekeza katika hoteli na utalii kwasababu ya faida zake kubwa za maendeleo, hasa kwa nchi za kipato cha chini na zilizoathiriwa na
migogoro.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates