Serikali imeobwa kutengeneza mpango mkakati kwa ajili ya wafanyabiashara utakao wawezesha kuwapatia mashine za kieletroniki(EFDs) bure ili kuweza kuweza kutumia mashine hizo ambapo kwa kufanya hivyo itasaida kuongeza na kukuza mapato ya taifa nchini.
Kwakufanya hivyo kutasaidia wafanya biashara wengi kuwa nazo kitu ambacho kwa sasa hawana kutokana na gharama kubwa ya ununuzi wa mashine hiyo hata kusababisha wafanyabiashara wengi kukwepa kutoa risiti kwa sababu hawanapesa ya kwenda kununua
katibu mwenezi wa chama cha Ada –tadea Taifa Zuberi Mwinyi alipokuwa akiongea na vyombo vya habari ambapo alibainisha kuwa serikali imekuwa inapoteza mapato mengi kutokana na wafanya biashara wengi kutotoa risiti kwakukosa mashine hizo za EFDs kutokana na mitaji yao kuwa midogo ingawa biashara zinaendelea
Alisema kuwa gharama za mashine hizo ni kubwa sana kwani kwa mashine moja inapatikana kwa kiasi cha shilingi laki nane (800000) jambo ambalo kwa mfanyabiashara mdogo inakuwa ngumu kununu mashine hiyo.
Alifafanua kuwa iwapo serikali itatoa bure mashine hizo kila mfanyabiashara ataweza kuichukuwa na kuiatumia na kama itashindikana kutoa bure basi wapunguze gharama za utoaji wa mashine hizo ,gharama ambazo watazipanga ziwe rafiki kwa kila mfanyabiashara na aweze kuzimudu.
Aidha aliwataka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kutoa elimu kwa ya kutosha kwa wafanya biashara na wasiishie kutangaza kuwa wanatoa elimu wakati wamekuwa hawafanyi hivyo kwa vitendo kama wanavyosema ,huku akiongeza uwa elimu ya kutosha ikitolewa pia itasaidia wafanyabiashara kujua umuhimu wa kulipa kodi .
Alisema kuwa iwapo mashine hizo zitatolewa zitolewe katika kila sekta ikiwepo ya usafirishaji mfano daladala zote ,mabasi makubwa ya usafirishaji mikoani,wamachinga ,wenye maduka, ikiwemo wa mabango, na pindi wanapopewa wakipangiwa viwango vya siku itasaidia kukusanya fedha nyingi
Aidha pia aliwataka maafisa wa TRA wanapotembea katika mitaa mbalimbali kukusanya kodi ya mapato wawashirikishe na viongozi wa mitaa hilo ili kuweza kurahisha zoezi hilo ,kwani viongozi hao ndio wanajua wafabiashara waliopo katika mitaa yao .
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia