Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKAMBA AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI WA SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI(TPDC)

wajumbe wa bodi ya TPDC wakiwa katika picha ya pamoja na waziri wa nishati January Makamba mara baada ya bodi hiyo kuzinduliwa rasmi Leo July 4 jiji Arusha
 

Na Woinde Shizza,Arusha

Waziri wa Nishati January Makamba amesema uendeshaji umahiri na umadhubuti wa uongozi wa shirika la TPDC, ni Jambo ambalo serikali unalipa uzito wa hali ya juu.

Makamba Ameyasema hayo wakati akizindua bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo jijini Arusha na kueleza kwamba uteuzi wa bodi hiyo unaakisi dira na Malengo mapya ya serikali kwa shirika hilo kuelekea katika mafuta na gezi.

Amesema bodi hiyo chini ya mwenyekiti wake balozi Ombeni Sefue inakidhi nafasi ya TPDC katika maendeleo ya nchi, Dira na mwelekeo mpya wa TPDC katika uchumi mpya wa Gesi na maendeleo ya mafuta nchini kwa ujumla.

"Dhamira yetu ni kuona shirika hili linatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi na sio katika mapato tu bali uendeshaji wa rasilimali watu katika tasnia hii lakini pia ushiriki wa nchi katika miradi mikubwa ya kimkakati ya mafuta na Gesi" Alisema Makamba


Wajumbe wa bodi wakiwa katika kikao Cha uzinduzi huo
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi hiyo ya TPDC Balozi Ombeni Sefue ambaye pia ni katibu mkuu Kiongozi mstaafu amesema wao kama bodi kazi yao ni kwenda kuchangamsha na kuhakikisha kila kitu kinaenda inavyotakiwa na sekta hii ili taifa liweze kunufaika na rasilimali zake za mafuta na Gesi tulizopewa na Mungu.
 Waziri wa nishati January Makamba akiongea wakati wa uzinduzi wa bodi ya TPDC Leo jijini Arusha 

Mikakati iliyopo kwa sasa ni ile ya serikali na haijaanza leo tutaipitia kama bodi mpya tumefanikiwa wapi na changamoto ni zipi na zitatatuliwaje ili kazi iendelee vizuri kujenga TPDC yenye kusaidia serikali.

Awali Mkurugenzi wa Shirika la mafuta na Gesi nchi muhandisi James Maragio amesema kuwa miradi ya mafuta na Gesi itakapokamilika itasaidia kutatua changamoto za wananchi.

Alisema kuwa wana miradi mikubwa ikiwemo mradi wa bilion 40 ikiwemo mradi wa kujenga bomba la mafuta kutoka hoima Uganda ambao umeonyesha mafanikio pia kuna maradi wa kutafuta mafuta katika bonde la ufa ambao upo kwenye Mchakato. 

 Picha wajumbe wa bodi ya TPDC wakiwa katika picha ya pamoja na waziri wa nishati January Makamba Leo mara baada ya kuzindua bodi hiyo.

Naye Mkurugenzi wa mamlaka ya udhibiti wa mafuta na Gesi nchini (PURA),Mhandisi Charles Sangweni alisema kwamba uundwaji wa bodi ya TPDC utaleta tija na kusaidia shughuli za Utekelezaji ndani ya serikali na kuongeza kuwa shughuli nyingi hapo awali kama maamuzi ndani ya PURA zilikwama Kutokana na kukosekana kwa bodi hiyo

Post a Comment

0 Comments