BREAKING NEWS

Monday, July 18, 2022

WATANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKI KWA WINGI KATIKA ZOEZI LA SENSA YA MAKAZI NA WATU

 

Na Woinde Shizza,ARUSHA

 




 

Wananchi wametakiwa kushiriki kwa wingi katika  zoezi  la  Sensa   ili  kuweza kusaidia serikali    kufikia malengo  ya kujua idadi ya watu na makazi ambayo itaweza kuhisaidia  kurahisisha utoaji  wa huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi wake .

 

Hayo yameeelezwa na katibu  mwenezi  taifa wa chama cha siasa cha ADA-TADEA Zuberyi Mwinyi wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ambapo alibainisha kuwa zoezi hilo la Sensa ni muhimu sana kwani hata katika vitabu vya dini imeandikwa  na hata mitume ya zamani  walifanya sensa zao kabla ya kuingia kwenye vita ili kupata idadi ya jinsi gani wataweza kupigana vita na kuweza kushinda .

 

Alisema  zoezi la sensa ni zuri kwani linaweza kuisaidia serikali kujua idadi halisi ya wananchi wake  ambapo  kutokana na idadi hiyo itaweza kufikisha huduma muhimu kwa wananchi wake kutokana na idadi iliopo  ambayo pia itaweza kuongoa udanganyifu kwa unafanywa na badhi ya viongozi ambao sio waaminifu .

“ zoezi hili litasaidia sana kuwabana wale viongozi ambao sio waadilifu wanaotumia idadi ya watu katika kufanikisha mambo yao kwa kudanganya hesabu ambazo sio sahihi  katika utoaji wa huduma ili wafikie malengo yao katika kuibia serikali   kwa mfano sehemu ambayo inaitajika kujenga hospitali  wilaya inajengwa zahanati kutokana na udanganyifu wa kutofahamika idadi ya watu watakaopata huduma ndani ya sehemu husika “alisema Zuberi

Aliwasisitiza viongozi wa dini kuhakikisha wanawahamasisha waumini wao kushiriki katika zoezi hili ambalo ni muhimu sana katika jamii yetu ambalo litatusaidia kujua idadi ya watu ambayo itaweza kupatiwa huduma halisi na serikali na kwa muda stahiki

“kuna baadhi ya viongozi wa dini katika sensa iliopita walishawishi  baadhi ya waumini wao kutojitokeza pamoja na kushiriki katika zoezi hili kitu ambacho ni dhuluma kubwa sana hata kwao kwani watakuwa wanapata kitu ambacho hakipo katika mahesabu na sio halali kwao  kwakuwa hawajahesabiwa maana hata  dini inasema kitu ambacho hakipo tofauti na mungu ni haki  kifanyike kwa ajili ya faida ya wahusika waweze kujihudumia “alibanisha

 

Alibainisha viongozi wa dini wanamamlaka kubwa na  uwezo mkubwa wa kuweza kushawishi waumini wao hivyo ni vyema wakatumia nafasi zao kumuunga mkoano Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu na serikali yake katika kufanikisha zoezi hili la sensa ya watu na makazi kwani Tanzania imepata bahati kubwa ya  kiongozi mwanamke ambaye anamaono ya kuifikisha nchi yetu mbali.

 

 

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates