WANANCHI WA AFRIKA KUSINI WAENDELEA KUMUOMBEA MANDELA


Wananchi wa Afrika Kusini wanashirki maombi ya kitaifa ya mwendazake Nelson Mandela.
Siku hii ya maombi imesemekana kua siku ya kumkumbuka Mandela na maisha yake.
Rais Jacob Zuma atahudhuria maombi hayo katika kanisa la Methodist mjini Johannesburg, wakishirikiana na viongozi wengine kutoka dini mbali mbali kwa maombi yatakayofanyika siku nzima leo.
Maombi maalum ya kitaifa yatafanyika siku ya Jumanne kabla ya kufanyika mazishi ya kitaifa Jumapili tarehe 15 Disemba.
Wananchi wa Afrika Kusini wamekuwa wakikesha tangu Mandela kufariki siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 95.
Rais Jocob Zuma amewataka wananchi kwenda katika viwanja vya michezo , makanisa, kumbi mbali mbali na sehemu zingine zote za maombi, Leo Jumapili, kumkumbuka Mandela.
"Wakati huu tunapoomboleza kifo cha Mandela, tunapaswa kuwa pia tunaimba kusherehekea maisha yake kwa juhudi za mageuzi alizozifanya na kutuletea maisha mapya, tumuimbie Madiba,’’ alisema Rais Jacob Zuma.
Mrithi wa Mandela alipoondoka mamlakani, Thabo Mbeki, atahudhuria maombi katika kanisa ya Oxford Shul synagogue mjini Johannesburg mchana wa leo.
Viongozi wengine wakuu wa ANC, watahudhuria maombi katika maeneo mengine kote nchini humo,

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post