Jumla ya madawati 30 yametolewa katika shule ya awali ya Tegemeo iliyopo katika mtaa wa Eng'avunet katika kata ya Terati mkoani Arusha.
Akikabithi msaada huo wa madawati mkuu wa kitengo cha masoko na mahusiano katika banki ya KCB Christina Manyenye amesema huu ni mfululizo ambao banki yao imejipanga kufanya kwa mwaka huu.
Amesema kuwa teyari wameshatoa msaada katika mikoa ya Dar es salaam na Morogoro na mkoani kilimanjaro na sasa wamekuja kutoa mkoani Arusha ikiwa ni sehemu zote wanamatawi ya banki yao.
Alisema kuwa kwa upande wa mkoa wa Arusha wameamua kutoa msaada wa madawati katika shule hiyo kutokana na walitembelea eneo hilo na kukuta wanafunzi wakisomea chini hivyo banki yao ikaamua kuwapa madawati ili waondokane na matatizo ya kukaa chini.
Alisema kuwa mbali na kusaidia shule hiyo madawati pia wamewajengea madarasa ambayo hawajayakabithi rasmi mpka wayamalize kuyatengeneza .
"mmoja wa wafanyakazi wetu alitembelea eneo hili ndipo akakuta wanafunzi wakisomea chini ya mti ndo akaja akasema ofisini nasi kwa kuwa banki yetu inatoa pia huduma za kijamii tukaamua kuja kuwajengea darasa hili na pia kuwaletea madawati"alisema Manyenye.
Akipokea msaada huo mlezi wa watoto hao ambaye pia ni muahasisi wa kikundi cha kina mama cha ZINDUKA Rashmi Mattappally alisema kuwa anapenda kuwashukuru sana banki hii kwa msaada waliotoa kwani wao wenyewe watoto wao walikuwa wanaenda mbali sana kupata elimu na pia walikuwa wanasomea chini ya mti.
"unajua tunapenda kuwashukuru sana hii banki kwani kabla ya wao kuja kutujengea hili darasa tulikuwa watoto wetu wanasomea chini ya mti tulikuwa hatuna ubao wala nini watoto wanatumia vijiti kujifunzia kuandika "alisema Mattappally
Alisema kuwa wao kama wakina mama wa mtaa wa Eng'avunet waliona watoto wao wanaenda kusoma mbali ndipo wakaamua kutafuta mwalimu wa hapo hapo mtaani na kumuomba aanze kuwafundisha watoto hao.
"watoto walikuwa wanaeda kutafuta elimu mbali wengine hata walikuwa awaendi shule hivyo tukaamua kutafuta mwalimu na bahati nzuri balozi wetu akatosaidia akatupa haka kasehemu ndipo tukaanzisha darasa na mungu alivyo mkubwa akasaidia tukapata na wafadhili hawa KCB na kutujengea eneo"alisema Mattappally.
Shule hii ya Tegemeo inajumla ya wanafunzi 55 wa shule ya awali na la kwanza na inafundishwa na mwalimu mmoja aliyejitolea.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia