BREAKING NEWS

Monday, November 15, 2010

TERRY SAVELLE FOY AKIKABIDHI MAHINDI NA MAHARAGE KISONGO




Zaidi ya magunia 100 ya mahindi yametolewa kwa wananchiwanaoishi katika mazingira magumu wa kijiji cha lopilukuny katika kata ya Kisongo kilichopo katika wilaya ya Arusha .

Msaada huo ambao umetolewa na Huduma ya Jerry Savelle ya nchini Marekani ikishirikiana na ya nchini Tanzania(JMSMI) imetolewa juzi ikiwa wakiwa nalengo la kuwasaidia wananchi wanaoishi katika mazingira magumu wakiwemo watoto yatima pamoja na wamama wajane.

Akikabidhi msaada huo makamu wa rais wa huduma hiyo Terry Savelle Foy alisema kuwa huduma yao ambayo ipo marekani ikishirikiana na tawi lao lililopo hapa Tanzania ambao makao makuu yake yako mjini hapa wameona ni vyema kujitoa na kuwasaida wananchi ambao wanaishi katika mazingira magumu na hii ni mara yao ya pili kutoa msaada kwa wananchi hawa.

Alisema kuwa hii ni mara yao ya pili kutoa msaada kama huu kwani mwaka jana pia walikuja na kutoa misaada kama hii ya mwaka huu.

Alibainisha kuwa misaada waliyoitoa kuwa ni mahindi magunia 120 maharage magunia 50,mafuta ya kupikia katoni 50,pamoja na chumvi katoni 20 ,viatu vya watoto wa shule ambao wanaishi katika vituo vya kulelewa pamoja na mashuka ya kimasai ya kujifunika 150.

Aliongeza kuwa wao wameguswa kuona mazingira wanayoishi yatima pamoja na wajene hivyo wameamua kuja kuwapa japo kidogo ambacho mungu amewapatia ili kuweza kuwanusuru japo kidogo katika mazingira ambayo wanaishi.


Akipokea msaada huo mwenyekiti wa kijiji cha Lopilukuny Saitabau Namoyo alisema kuwa yeye binafsi anapenda kuwashukuru sana wageni hao kwa kuwaletea msaada huo kwani wamewaletea amsaada huo wakati unaostaili.


Alisema kuwa msaada huo utawasaidia kwa kiasi kikubwa kwani katika kijiji chao wamekuwa na tatizo la chakula kutokana na kutopata mavuno katika msimu uliopita.\


"Tunawashukuru sana hawa wageni wetu kwani wamaeleta msaada huu katika muda muhafaka kwani tulikuwa tunakabiliwa na tatizo la njaa sana katika kipindi hichi kwani sisi hatukubahatika kupata chakula katika msimu uliopita"alisema Namoyo


Alisema kuwa kwa msaada huu wanatarajia kugawa katika kaya 106 zilizopo katika kijiji chao na kubainisha kuwa wataanza kuwagawia wajane ,yatima pamoja na wale wananchi ambao wanaishi katika mazingira magumu sana.


Mbali na kijiji hichi huduma hii pia iligawa vyakula ikiwemo sukari na mchele katika vijiji vingine ambavyo waligawa viatu vya shule katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Seeway kilichopo katika kujiji cha kikatiti pia waliwagawa chakula ikiwemo sukari ,mchele ,unga na mafuta katika kikundi cha wakina mama wajane Kiwahumu kilichopo katika kijiji cha Nkwaranga.

Mbali na kutoa msaada huduma hii ya Jerry Savelle Ministry pia imeandaa mkutano mkubwa wa neno la mungu ambao utafanyika kwa muda wa siku mbili katika uwanja wa Arusha meru uliopo jijini Arusha.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates