Waziri wa zamani wa Ulinzi wa Rwanda, Jenerali Emmanuel Habyarimana ambaye mwaka 1999 alitoa ushahidi wa maandishi kwamba wanamgambo wa Interahamwe wa chama tawala cha MRND walifadhiliwa fedha, kupewa mafunzo ya kijeshi na silaha zikiwemo bunduki na mabomu, Alhamisi wiki hii aliukana ushahidi huo na kuuita ‘’propaganda.’’
Jenerali huyo alikuwa anamtetea Rais wa chama hicho, Mathieu Ngirumpatse anayeshtakiwa katika kesi moja na Makamu wake wa Rais, Edouard Karemera ambaye tayari amehitimisha utetezi wake.
‘’Nimehakiki taarifa hizo na kugundua kuwa zinashahabiana na ukweli uliopo. Baadhi yake zilithibitishwa na nyingine hazikuthibitishwa,’’ Jenerali Habyarimana aliiambia Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) wakati wa kuhojiwa na mwendesha mashtaka, Don Webster.
Katika ushahidi wake wa maandishi alioutoa kwa mwendesha mashtaka Oktoba, 1999, katika kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Waziri wa zamani wa Vijana, Callixte Nzabonimana, Jenerali huyo alieleza kwamba Interahamwe walifadhiliwa, kupewa mafunzo ya kijeshi na silaha na Wizara ya Vijana.
‘’Taarifa nilizonazo sasa ni tofauti na hali halisi ilivyokuwa,’’ aliiambia Mahakama iliyokuwa inaongozwa na Jaji Dennis Byron ingawaje alidai kwamba ushahidi wake wa 1999 ulitokana na matukio aliyoyashuhudia na kuishi nayo.
‘’Watu kama Nzabonimana walipandikiza mbegu za mauaji ya kimbari. Kama mtu huyu na wengine wenye nafasi kama yake wangekataa mauaji ya kimbari, kusingekuwapo mauaji ya kimbari,’’ sehemu ya ushahidi wake wa maandishi ulieleza, huku akitoa wito kwamba watu wa aina hiyo hawana budi kuadhibiwa.
Alipotakiwa kutoa taarifa anazodai alizipata baada ya ushahidi wake wa maandishi na ambao umemfanya sasa abadilishe ushahidi wake, shahidi huyo alianza kuelezea taarifa nyingine zinazohusu kundi la zamani la Waasi la RPF, ambao sasa ni watawala wa Rwanda na ambao hakuwahi kuwataja katika ushahidi wake wa awali.
‘’Nilikuwa na maoni fulani juu ya taarifa nilizopata wakati ule. Nilizieleza kama ni za kweli. Lakini baada ya utafiti niligundua kwamba ni tofauti,’’ alidai shahidi huyo.
Alipokuwa anahojiwa kwa mara ya pili na Wakili Msaidizi wa mtuhumiwa, Frederic Weyl ambaye pia alimwuliza swali kama hilo , Jenerali Habyarimana alisema ushahidi wake uliibuka na kushawishiwa na propaganda za vyombo vya habari na RPF.
Shahidi huyo alikwenda uhamishoni nchini Uswisi baada ya kutofautiana na Rais Paul Kagame. Jenerali huyo alitumikia serikali ya Kagame katika nafasi mbalimbali nyeti nchini mwake kati ya 1995 na 2003 alipoikimbia nchi hiyo.
Viongozi hao waandamizi wa MRND wanashtakiwa kwa tuhuma saba ikiwa ni pamoja na mauaji ya kimbari, kula njama kufanya mauaji hayo, kuchocheo mauaji hayo na uhalifu dhidi ya ubinadamu unaodaiwa kufanywa na wanachama wa chama chao pamoja na wanamgambo wao wa Interahamwe.