WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema serikali imeandaa mipango ya kuwa na utaratibu mzuri wa kuwawezesha wakulima kupata mikopo kutokwa kwa benki ya kilimo inayotarajiwa kuzianzishwa pamoja na katika benki zingine za biashara.
Pinda alisema hayo mjini hapa wakati akifungua Mkutano wa 15 wa Taasisi za Fedha, ambao umewahusisha wataalam mbalimbali wa fedha, wasomi, watunga sera, wataalamu wa benki na wadau wengine kutoka ndani na nje ya nchi.
“Tunakuna na utaratibu utakaowawezesha wakulima kupata kirahisi mikopo na kuitumia kwa ualishaji,” alisema Pinda na kusisitiza, katika taratibu hizo mpya za utoaji wa mikopo, wakulima watapata pembejeo na vifaa vingine, badala tu ya kuwapatia fedha taslimu.”
“Hatutaki wakulima wapewe fedha taslimu mkononi, badala yake wapate mikopo hiyo kwa njia ya mbolea, dawa za kuulia wadudu, matrekta na vitu vingine,” alisema.
Alieleza kwamba wakulima wanatakiwa kuwezeshwa namna ya kutumia vema mikopo yao ili benki ziweze kurejeshewa fedha zao.
“Nidhamu katika kutumia mikopo ya benki ni ndogo sana kwa watu wengi wakiwemo wakulima, ndio maana tumeona ni vema wakiwezeshwa kupitia zana za kilimo na pembejeo,” alisema.
Alisema chini ya mkakati mpya, wakala wa kilimo na makampuni yanayojishughulisha na zana za kilimo yatawezeshwa ili wakulima wapate kile wanachokihitaji kutoka kwao.
Akitoa mfano, Pinda alisema, “kama mkulima anahitaji mbolea ya chumvi chumvi anaweza kuwasilisha ombi lake ili kupata bidhaa hiyo kupitia kiwandani ambako atakopeshwa, na vile vile katika vifaa vingine.
Alisema lengo hilo ni kuhakikisha wakulima wanajihusisha kikamilifu katika uzalishaji na wakati huo huo, benki ziendelee na majukumu yake na mwisho wa siku taifa linaweza kupata mafanikio.
Gavana wa Benki Kuu Tanzania, Profesa Benno Ndulu alisema ajenda kuu ya mkutano huo wa siku mbili ni kuhusu kuwa na muungano wa sarafu ya pamoja katika Afrika Mashariki na matokeo yake katika msimamo wa kifedha.
Alisema wazo la mkutano huo ni kuzungumzia namna nzuri zaidi namna umoja huo wa fedha unaweza kufanya kazi katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia