SIJAONA VIWANGO

Kocha mkuu wa timu ya taifa Jan Poulsen amesema kuwa ajaona viwango katika timu ya AFC na Kagera sugar wakati alipokuwa akiangalia mechi ya mwisho ya mzunguko wa kwanza ambayo ilizikutanisha timu hizi mbili.

kocha huyo aliyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari katika uwanja wa Sherk Amri Abeid mara tu ya mechi hii kumalizika ambayo timu ya AFC iliweza kuendelea kuwakatisha tamaa washabiki wao mara baada ya kufungwa magoli matatu kwa limoja katika uwanja wa nyumbani.

Alisema kuwa kwa upande wa timu ya AFC ya jijini Arusha inatakiwa kujitaidi sana kwani mwanzoni mwa mchezo walionekana kumletea matumani kwani walikuwa wanashambulia vilivyo lakini mwishoni walilegea na kuishiwa nguvu.

Kwa upande wa timu ya Kagera Sugar alisema wachezaji ni wazuri na wanastamili mchezo kwani japokuwa walikuwa ugenini lakini waliweza kuonyesha kandanda zuri ila bado katika timu hizo ajaona mchezaji wa kumchukuwa.

Alisema kuwa wasikate tamaa kinachotakiwa ni kujituma na kujitaidi zaidi ili katika mzunguko wa pili washinde na aweze kupata wachezaji ambao atawachagua kwa ajili ya timu yataifa.

katika mechi hii timu ya Kagera Sugar iliweza kufanya vyema mara maaba ya kujipatia magoli matatu ambapo katika goli la kwanza lilifungwa na Ally Lundenga kunako dakika ya 3 katika kipindi cha kwanza huku goli la pili likiingizwa kimnyani na Gaudence Mwaikimba dakika ya 35 na goli la tatu likifungwa na Saidi Dilunga mnamo dakika ya 73 ya kipindi cha pili.

kwa upande wa timu ya AFC mchezi ambaye alibahatika kuipatia timu yake goli la kufutia machozi ni Jummy Shoji ambaye aliingiza goli katika dakika ya 25 ya mchezo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post