Shule ya Sekondari na chuo cha ualimu ya Bishop Durning iliyopo eneo la Sanawari ya juu Mkoani Arusha inajipanga kuanzisha chuo kikuu ndani ya miaka 5 ijayo ili kuinua na kuboresha kiwango cha elimu ili kuendana na soko la ushindani kimataifa
Akizungumza wakati wa mahafali ya nne ya wahitimu wa kidato cha nne Mkuu wa shule hiyo Bw Lomunyaki Pipiyo amesema pamoja na shule hiyo kusaidia watoto 30 wasio na uwezo kusoma bure pia iko kwenye mchakato wa kujipanga na kuanzisha chuo kikuu
“Pamoja na kuwa tayari tunayo shule ya Sekondari yenye kidato cha kwanza hadi cha sita na chuo cha elimu ambacho kilianza rasmi Julai mwaka huu pia tunajiandaa kuanza Ujenzi wa chuo kikuu”alisema Bw Lomunyaki
Aidha katika risala yake wakati wa mahafali hiyo alisema kuwa shule hiyo yenye wahitimu 57 ambao ndio wamehitimu ilianza mwaka 2004 na imekuwa na kiwango cha kufaulisha wanafunzi kitaifa kwa asilimia 80%
Aliongeza kuwa kiwango cha elimu itolewayo shuleni hapo imesaidia wanafunzi wengi kufaulu ambapo wengine wapo nje ya nchi kama Uingereza wakiendelea kusoma wakati baadhi yao wakiwa tayari ni wafanya kazi katika nchi hiyo
Aliendelea kubainisha kwamba tayari wamenza mchakato wa kupata zaidi ya Ekari 100 katika eneo la kisongo na kwamba hadi kufikia mwezi march 2011 watakuwa wameshakamilisha taratibu za kiwanja na kuwa tayari kwa kuanza hatua za ujenzi
“Tunakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kutokuwa na maabara kwa ‘O’level hali inayopelekea kutumia maabara ya ‘A’level, kutokuwa na Zahanati kwa ajili ya huduma ya afya hivyo tunahitaji ushirikiano zaidi wa Serikali na wadau mbali mbali”alisema Bw Lomunyaki
Naye mgeni rasmi wa mahafali hiyo Bw Tojo Abdi ambaye ni diwani wa kata ya kati amewataka wahitimu hao kufanyia kazi elimu waliyoipata shuleni hapo na kuacha kuhadaika na tamaa za mwili zitakazoweza kupunguza kasi ya elimu yao
Kwa upande wao wahitimu wamesema wanashukuru uongozi wa shule hiyo kwa kuwapa elimu bora na ushirikiano mzuri wa upendo baina ya walimu wao na kuahidi kuwa wataifanyia kazi elimu hiyo bila kukata tamaa huko waendako