No title

WANACHAMA wa klabu ya wazee ya jijini Arusha wamefanya uchaguzi mkuu wa kuwachagua viongozi wa klabu hiyo huku wanachama hao wakimchagua mwanahabari mkongwe nchini ,Danford Mpumilwa kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo kwa miaka mitatu ijayo.





Pia wanachama hao walimchagua,Aatsa Atogo kutoka nchini Cameroon kushika nafasi ya mwenyekiti msaidizi ,Ally Mamuya(Tanzania) kushika nafasi ya katibu ,Saidou Guindo(Mali) katibu msaidizi,Ernest Olomi(Tanzania),Mhasibu ,Sophia Burra(Tanzania) mhasibu msaidizi ,Emmanuel Ntoko(Cameroon),Afisa mahusiano na mshahuri wa masuala ya kisheria ,Francis Kiwanga(Tanzania).




Klabu hiyo yenye zaidi ya wanachama 150 imewaunganisha wanachama wanaotumikia nafasi mbalimbali jijini Arusha wakiwemo watumishi wa kimataifa,wanasiasa,wafanyabiashara,walimu ,maafisa wa mashirika ya kiserikali na binafsi sanjari na wakurugenzi wa makampuni mbalimbali nchini kwa shughuli za kimichezo.




Pia klabu hiyo inajihusisha katika kuinua sekta ya michezo nchini ikiwa ni pamoja na kusaidia na kuboresha shughuli mbalimbali za kimichezo kwa watoto na watu wazima mkoani Arusha.





Akihojiwa mara baada ya kuchaguliwa Mpumilwa alisema ya kuwa klabu hiyo itaendelea kuinua sekta ya michezo mkoani Arusha huku akiushukuru uongozi wa chama cha wakulima kanda ya kazkazini(TASO) kwa kuwapatia eneo la makao makuu ya klabu hiyo ndani ya viwanja vya nane nane jijini hapa.




“Nashukuru sana kwa kuchaguliwa tena kuiongoza klabu hii lakini shukrani zaidi ziende kwa TASO kanda ya Arusha kwa kutupatia eneo la kujenga makazi ya klabu yetu kwani tayari ramani ya mchoro wa eneo umekamilika michango ya fedha na vifaa vinamiminika kwa wingi tu”alisema Mpumilwa

Awali kabla ya uchaguzi huo wanachama wa klabu hiyo walishuhudia mechi za chini ya umri wa miaka 14 na 12 kati ya Future Stars Academy na Twin Bridge Stars ya Daraja Mbili huku kikundi cha ngoma kutoka jeshi la kujenga taifa cha (JKT Oljoro Dancing Group) kikuwatumbuiza mamia ya wanachama wa klabu hiyo katika uchaguzi huo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post