MWANANDOA ADAIWA KUTISHIA MKEWE KWA KISU, ATEMBEZA MKONG’OTO KWA WATOTO WAKE

Mwanandoa aliyefahamika kwa jina la Kelvin Temu amedaiwa kumtishia mke wake kwa kisu Bi Daines Nkini kwa lengo la kutaka kuoa mwanamke mwingine wa kisambaa kwani mkewe huyo hampi pesa za matumizi yake binafsi ya unywaji wa pombe.



Akizungumza mke wa mwanandoa huyo Bi Daines Nkini amesema mume wake amekuwa akivumilia mateso ya unyanyasaji kwa muda mrefu tangu mwaka 2002 baada ya harusi yao mumewe alikuwa akimnyanyasa kwa kumtishia kumuua ili aweze kuoa mwanamke wa kisambaa



“Mimi ndio natafuta hela ya kutufanya tuishi na watoto wangu nawavalisha na kuwalisha mwenyewe wakati mume wangu hana kazi alifukuzwa kazi wakati alipokuwa akifanya kazi katika kampuni ya Abakombi mimi ndio mtafutaji wa riziki ya familia lakini ananinyanyasa mume wangu”alisema Bi Daines kwa uchungu.



Aidha Bi Daines alionyesha nakala na kumpatia mwandishi wa habari hizi zikionyesha mume wake alivyokuwa anakiri na kumuomba mkewe amsamehe na kwamba hatarudia kumfanyia vitendo hivyo viovu tena ambapo Bi Daines hakuwa tayari kutekeleza ombi hilo kwa wakati huu.



Aliongeza kuwa mgogoro huo aliufikisha polisi ambapo polisi kupitia Afisa wake aliyefahamika kwa jina la Fredirick Mrope aliwaita wote yeye na mumewe na kuwashauri wamuone mchungaji wao ili kuweza kutatua tatizo lao kisha taarifa za maamuzi zirejeshwe polisi.



Wakati huo huo Bw Kelvin alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na shutuma hizo za unyanyasaji dhidi ya mkewe alikanusha kutokumfanyia unyanyasaji huo ambapo barua zake za kukiri zinaonyesha kuomba radhi kwa vitendo alivyomfanyia mkewe



Katika maelezo ya Barua ya Bw Kelvin ambayo ilionyesha kukiri makosa yake ilimtaka Bi Daines mkewe aweze kumsamehe mumewe ili aweze kurejea kwenye ndoa bali Bi Daines hakuwa tayari kwa sasa na kudai kwamba anahitaji muda wa utulivu wa kumuomba Mungu wake ili aweze kuingilia kati ndoa yao



Hata hivyo baada ya kumuona mchungaji wao aliyefahamika kwa jina la Francis Letara alimtaka kila mmoja aweze kumuandikia barua ya maelezo pamoja na maamuzi ili aweze kufikisha kwa ajili ya kuziandaa kwa pamoja ili kuziwasilisha polisi

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post