No title

TIMU ya JKT Oljoro ya jijini Arusha leo imeweza kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Sherk Amri Abeid mara baada ya kuweza kuwanyuka mikwaju mitatu bila timu ya Polisi Morogoro.



Timu hii ya Jkt Oljoro ambayo ipo katika ligi daraja lakwanza imeweza kujiongezea pointi na kujikuta wamefikisha jumla ya pointi tisa mara baada ya kuweza kufunga magoli matatu ambayo kati ya magoli hayo goli moja waliweza kulipata kwa ulaini mara baada ya mchezaji wa Polisi morogoro kujifunga mwenyewe.



Katika mechi hiyo mchezaji wa timu ya Jkt Oljoro aliyejulikana ikwa jina la Amor Janja aliweza kuiandikia timu yake goli la kwanza kunako dakika ya tisa ya mchizo huku katika dakika ya 38 ya mchezo mchezaji wa timu ya polisi morogoro Shomari Kapombe aliweza kujifunga mwenyewe katika lango lao na kuisababishia Jkt oljoro hadi kufikia mapunziko kukuta wakiongoza kwa magoli mawili huku polisi morogoro wakitoka kapa.



Waliporudi kutoka mapumziko timu ya Polisi Morogoro waliongeza nguvu lakini hazikuzaa na ilipotimu dakika ya 75 ya mchezo mchezaji wa polisi morogoro alicheza rafu na kusababishia timu ya Jkt Oljoro kupata goli kwa njia ya penati ambapo Iddi Salehe aliweza kupiga vyema na kuisababishia timu yake kupata goli la tatu.



hadi kipindi kumalizika timu ya Jkt Oljoro ilijikuta ikiondoka uwanjani na magoli matatu huku wakifikisha pointi tisa na Polisi Morogoro ikiambulia patupu na kubakia na pointi zao sita.



Gazeti hili lilizungumza na kocha wa timu ya Polisi Morogoro John Tamba naye alisema kuwa kufungwa ni matokeo na asiyekubali kufungwa sio mshindani.



Alisema kuwa mchezo ulikuwa ni mzuri na aliwasifia waamuzi wa mchezo huo na kusema kuwa walifuata taratibu zote za kimchezo na kusema kuwa kwa upande wa mapungufu aliyokuwa nayo atayarekebisha.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post