MSUMARI AFURAISHWA NA BAADHI YA VIONGOZI WA MICHEZO KUTWAA NAFASI ZA UBUNGE

MWENYEKITI wa matawi ya Klabu ya Simba mkoani Tanga,Mbwana Msuamari kufurahishwa na kitendo cha viongozi wa michezo kutwaa nafasi za Ubunge akisema kwamba anaamini mataleta mabadiliko makubwa.



Msumari ambaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juzi alisema ushindi wa Ismail Aden Rage,Juma Nkamia na Profesa maji Marefu (Stephen Ngonyani) anaamini utaleta mabadiliko makubwa katika medani ya michezo nchini.



Alisema kwamba kitendo cha kuingia bungeni kwa Profesa Maji Marefu,Rage na Nkamia kutaleta mabadiliko makubwa kwani wataweza kutoa ushauri na kuchanganya mawazo yao katika kusaidia kwa hali na mali katika kuinua michezo hapa Tanzania.



“Nkamia,Profesa na Rage ni watu safi katika michezo wote kwa ukereketwa wao watatuletea mabadiliko makubwa katika michezo hivyo tunafurahia ushindi wao kwa vile tunaamini wataleta mabadiliko makubwa kwenye michezo hapa nchini”alisema Msumari.



Akielezea uzoefu wao kwenye michezo,Msuamari alimtaja Profesa Majia Marefu kwamba ni mtu muhimu ambaye ameweza kujitoa kuifadhili Simba ya jijijini Dar es salaam na klabu ya Coastal kiasi cha kuziwezesha kufanya vizuri katika ligi kuu.



Kwa upande wa Rage,Msumari alisema amewahi kushika nyadhifa kubwa tangu enzi za FAT hadi sasa TFF ambapo atatumia uzoefu wake katika kuhakikisha medani ya michezo hususani soka inasonga mbele na kuliletea Taifa hili sifa na matarajio lukuki kwa ushindi.



Akimzungumzia Nkamia,Msumari alisema,anaweza kutumia taaluma yake ya mambo ya habari katika kuhakikisha soka na michezo ya Tanzania inasonga mbele kwa maelezo kuwa ana upeo mkubwa katika medani hiyo ya michezo kitaifa na kimataifa.



Ismail Aden Rage,Juma Nkamia na Profesa Maji Marefu ni wabunge waliopita kwa tiketi ya CCM ambapo wanaelezwa kuwa wadau muhimu katika michezo hapa nchini na wapenzi wa michezo wameelezea kupata maendeleo ya haraka katika sekta hiyo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post