Pilika pilika za kumpata kiongozi ambaye ataongoza jimbo la Arusha mjini zilianza jana na hadi kufikia leo asubuhi kulikuwa tayari wananchi wamesha wajua madiwani wa wa jiji la Arusha
Katika mchakato mzima wananchi wa jiji la Arusha baada ya kukuchwa leo kila mmoja alionyesha mori na hamu ya kumjua ninani ambaye amebahatika kuongoza jimbo lake la Arusha mjini hivyo basi wananchi wengi walijitokeza katika ofisi za Halimashauri ya jiji hili na kutaka kumjua yupi kiongozi wao ambaye amebahatika kuomuongoza.
Hivyo basi wananchi wengi walifika tangu asubuhi ya saa kumi na mbili kujua nani ni kiongozi walikaa ka muda mrefu wakisubiri kutangaziwa majibu lakini hawakuambulia kitu hadi pale jua lilipo zama ndipo wananchi hao ambao wengi wao walitokea katika vyama vya upinzani ambao walikuwa zaidi ya 5000 walipozidiwa na uzalendo kuwashinda ndipo wakaanza kupiga kelele na kusema wanataka majibu ya kura zao
"tunataka majibu yetu tunataka majibu yetu msipotupa tunaingia usipo tupa tunaingia "maneno hayo yalisikia yakisemwa na wananchi ambao walikuwa wanasubiria majibu ya kura zao tangu asubui
Kwa bahati nzuri joto lile liliwatishia wanatoa majibu akiwemo msimamizi wa uchaguzi na kufikia hatua ya kuharakisha majibu na kutoa kwa wananchi ambao walikuwa wakisubiri kwa muda mrefu wananchi ambao walikuwa na shauku ya kumjua mbunge wao.