Kanisa linalojulikana kwa jina la Heritage Of Faith Christian Centre (HFCC) limeandaa mashindano ya mpira wa miguu yanajulikana kwa jina la Revival Cup ambayo yameanza kutimua vumbi hivi karibuni katika uwanja wa Gymkana uliopo jijini hapa.
Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa na mratibu wa mashindano hayo Huruma Mzirai zinasema kuwa mashindano hayo yatashirikisha timu mbalimbali za makanisa na timu za mitaani .
Alisema kuwa mashindano hayo yatajumuisha jumla ya timu 12 za mkoani hapa na yatachezwa kwa mfumo wa ligi.
Alisema kuwa timu hizi zimegawanyika katika makundi matatu ambazo alitaja timu ambazo zipo katika kundi A ni Herotage,Engarenarok,N.L.O, pamoja na Weekend zingine zilizopo katika kundi B ni Pallot ,Ilboru,Kioga pamoja na Ilkidinga .
Kwa upande wa kundi C alisema zipo timu ya Oldonyosapuk ,Oloirowa,Shangilieni pamoja na Oloigero.
Mzirai alisema kuwa nia ya kanisa lao kuandaa mashindano haya ni kuwaleta vijana pamoja na kuwaelezea kuhusiana na swala zima la ugonjwa hatari wa ukimwi pamoja na kuwaelimisha vijana njia za kujiepusha na makundi maovu.
Alisema lengo lingine la mashindano haya ni kuwaeleza vijana jinsi ya kumtegemea mungu kama kijana na kujua msimamo wake na jinsi ya kufanya ili kujiletea maendeleo.
Alitaja zawadi ambazo zitatolewa katika mashindano haya kuwa ni kwa mshindi wa kwanza atapatiwa fedha taslimu kiasi cha shilingi laki mbili ,mpira ,jezi pamoja na kombe lenye dhamani ya shilingi laki tatu huku mshindi wa pili akiondoka na fedha taslimu kiansi cha shilingi laki moja pamoja na jezi na mpira na mshindi wa tatu ataondoka na kitita cha shilingi elfu hamsini pamoja na mpira
Alisema kuwa mpaka sasa timu nne zimeshacheza katika ligi hii na kutaja timu hizo ambazozilibahatika kufungua dimba la mashindano haya kuwa ni Hertage ambao walikutana na Engarenarok ambapo timu hizi zilijilazimu kugawana pointi mara baada ya kutoka sare ya bao moja kwa moja.
Kwa upande wa timu ingine alisema timu ya Pailot ilikutanishwa na timu ya Ilboru ambapo katika mechi hii timu ya Iliboru iliweza kuinuka kidedea cha goli moja bila.
Aliwa sihi wakazi wa mkoa wa Arusha na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano haya ambao fainali zake zinatarajwa kufanyaka katika uwanja wa mpira wa shule ya meru ambapo fainali hizo alibainisha zitaambatana na mkutano mkubwa wa neno la mungu ambao utashirikisha makanisa mbalimbali ya mkoa wa Arusha.