Diwani wa kata ya
Monduli mjini,(CCM),Isack Joseph maarufu kama Kadogoo “amemtolea uvivu” mwenyekiti
wa mtaa wa Sabasaba uliopo ndani ya kata yake,Charles Malaika katika mkutano wa
hadhara huku akimtuhumu kukwamisha utekelezaji wa ilani ya Chama cha CCM.
Mkutano huo ulifanyika
hivi karibuni ndani ya kata hiyo ambapo akizungumza na wananchi mbalimbali waliohudhuria
diwani huyo alimtuhumu Malaika kwamba ameshindwa kuwasilisha mpango kazi katika
mtaa wake hali ambayo inakwamisha maendeleo ya kata yake.
Diwani huyo kwa jazba
akiwahutubia wananchi wake alisema kuwa ni mtaa mmoja kati ya minne iliyopo
ndani ya kata yake haujawasilisha mpango kazi wake wa maendeleo hali ambayo
inakwamisha juhudi za maendeleo.
“Nina shaka na huyu
mwenyekiti wangu wa mtaa wa Sabasaba kwa kuwa haiwezekani wewe tu usiwasilishe
mpango kazi wako tofauti na wengine”alisema Joseph
Akijitetea katika
mkutano huo mwenyekiti huyo alidai kuwa mwingiliano wa majukumu ulimpelekea kutowasilisha mpango
kazi huo kwa wakati huku akitoa ahadi katika mkutano huo kuwasilisha mapema iwezekanavyo.
Katika hatua nyingine,diwani
huyo aliwaambia wananchi kuwa miongoni mwa masuala kama kuanzisha mfuko wa
kata,kusomesha watoto wasio na uwezo sanjari na kuhakikisha wananchi wanapata viwanja na kuanza ujenzi wa makazi ya
kudumu yametekelezwa kwa asilimia 95.
Alisema kuwa katika mwaka
wa fedha 2013/14 suala la ukarabati wa kituo cha mabasi cha Monduli mjini ,huduma
ya maji safi na salama pamoja na ujenzi wa barabara miradi hiyo inatarajia kukamiliki
kwa asilimia 100 na kuwataka wananchi wampe ushirikiano.