Mkazi wa Dar es Salaam akizungumza na wenye duka kandokando
ya barabara ya Uhuru Kariakoo jana ambao walifunga maduka yao kufuatia mgomo wa
wafanyabiashara kugomea mashine za TRA ambazo wanadai zinahitilafu nyingi.
Wengine walifungua maduka yao hivi.
Wateja walipita kutafuta huduma na kukereka kabisa
BBC ilifika Kariakoo na kuzungumza na baadhi ya wafanya biashara pamoja na wateja kupta maoni yao.
Wateja walizunguka na kuamua kukaa chini madukani.
Duka
hili wao waliamua kuendelea na biashara kwa kile walichosema kuwa hata
wakiwa katika mgomo bado watalazimika kulipa kodi. Hivyo ni bora
waendelee na biashara.
Jiji
la Dar es Salaam hususani eneo la Kariakoo jana wafanyabishara wake
katika maeneo hayo waliingia katika mgomo wa kutofungua maduka yao
kupinga mashine za kutolea risiti za elektroniki (EfDs) ambazo zipo katika mfumo wa uhakiki wa ukusanyaji kodi.
Wafanyabishara
hao wakizungumza na Father Kidevu Blog, wamesema mbali na mashine hizo
za EfDs lakini pia wamekuwa wakiongezewa kodi kila kukicha.
Wamesema
kuwa matatizo ya mashine hizo ya kuharibika mara kwa mara, kushindwa
kutoa mahesabu ya siku kwa wakati na kushindwa kuprint risiti ni kero
kwao.
Pichani juu ni Wafanya biashara wa maduka ya bidhaa mbalimbali katika
mitaa ya uhuru na Swahili Kariakoo, Shamun Qurban (kushoto) na mwenzake Murtaz
Abbas ‘Kokole’ wakisoma gazeti nje ya maduka yao waliyoyafunga jana kufuatia
mgomo wa wafanyabiashara kugomea mashine za TRA ambazo wanadai zinahitilafu
nyingi.