TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu Mkuu wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahaman Kinana amesikitishwa na taarifa ya
kifo Cha Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dr Sengondo Mvungi kilichotokea
Jana katika Hospitali ya Millpark nchini Afrika ya Kusini.
Kwa niaba ya
Chama Cha Mapinduzi, Katibu Mkuu anawapa pole wanafamilia, Mwenyekiti wa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba na Uongozi wa Chama Cha NCCR-Mageuzi.
Hakika Taifa limepoteza Mtaalamu wa Sheria, Kiongozi Mzalendo na hodari katika kipindi ambacho mawazo yake
yanahitajika kwa kiasi kikubwa kuliendeleza Taifa hili.
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu
mahali pema peponi.
Imetolewa na:
KATIBU WA
HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
13/11/2013