MASHUJAA KUWAPAGAWISHA WAKAZI WA ARUSHA


BENDI  mpya inayotamba kwa sasa hapa nchini na ambayo imechukuwa tuzo mbalimbali za muziki hapa nchini (MASHUJAA BAND) jumamosi  November 16  inatarajia kushuka jijini Arusha katika ukumbi wa triple A kuwapa burudani wakazi  wa jiji hilo na vitongoji  vyake.

Akiongea na waandishi wa habari muandaaji wa  onyesho hilo kutoka katika kampuni ya Rickenet Intertament Papa Ernest alisema kuwa bendi hii ya mashujaa itatua jijini hapa kwa ajili ya onyesho hilo ambapo alilifafanua kuwa tangu bendi hii kuanzishwa hii  ni onyesho lao la kwanza kufanya jijini hapa.

Alisema  kuwa bendi nzima ya mashujaa inatarajiwa kutia timu jijini hapa  wakiwa na wanamuziki wake wote ambapo aliwataja baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo kuwa ni pamoja na  Chaz Baba,

Alifafanu kuwa bendi hii imedhimiria ‘kufunika’ katika  onyesho hilo na wamejipanga  kufunika bendi zote ambazo zimeshawahi kufanya onyesho katika  jiji hili la  Arusha kwani bendi hii  ina historia nzuri katika muziki wa Tanzania  haswa katika maonyesho yao mbalimbali ambayo wameshayafanya hapa nchini.

Aidha Ernest alisema kuwa  ameamua kuwaletea wakazi hawa wa jiji la Arusha bendi hii kwani bendi hii imekuwa inafanya vyema katika tasinia hii ya muziki wa danci ambapo alifafanua kuwa  kwa mwaka huu bendi hii ya mashujaa inashikilia tuzo tano za muziki hapa nchini.

Alitaja kiingilio cha shindano hili ni shilingi10000 kwa kila mmoja  huku akiwasihi wakazi wa mkoa wa Arusha kujitokeza kwa wingi kuangalia bendi hii ambayo inawanamuziki wengi ambao wanajua kutawala jukwa a kwa kuimba pamoja na kucheza.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post