Ticker

6/recent/ticker-posts

CRDB YAKUZA KIPATO CHA FAMILIA



Meneja wa Benki ya  CDRB  tawi la Usa River  lilipo mkoani Arusha  Jenipher
 Tond akikabidhi zawadi ya tisheti kwa mtoto aliyeshinda kucheza mziki
leo sherehe
za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na
familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za wateja

 Watoto wakimkimbiza kuku katika mashindano yaliyofanyika kwenye sherehe za
siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na
familia za wafanyakazi wa benki pamoja na familia za wateja
 Malindi band ya mkoani kilimanjaro ikitumbuiza sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila
mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafanyakazi wa benki pamoja na familia
za wateja
Mfanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la USA akikabidhi zawadi kwa mtoto
Benki ya CRDB imeendelea kukuza kipato cha familia nyingi nchini za hali ya
chini ,kati na juu kwa kuwahimiza wateja wake kufanya uwekezaji wenye tija
pamoja na kujiwekea akiba kwa maisha ya baadae.
Hayo yameelezwa Meneja wa Benki ya  CDRB  tawi la Usa lilipo mkoani
Arusha  Jenipher
 Tond wakati wa maadhimisho ya siku ya Familia ya CRDB iliyofanyika katika
viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha na kuzikutanisha familia
mbalimbali za wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na familia za wateja wa
benki hiyo waishio jijini Arusha.
Meneja huyo amesema kuwa benki hiyo inaendelea kuhamasisha uwekezaji na
kutoa mikopo kwa ajili ya kukuza mitaji na kuinua pato la mwananchi mmoja
mmoja hadi kwa taifa.
Meneja wa benki hiyo tawi la Meru Leonce Mathey amesema kuwa benki hiyo
imesogeza karibu huduma kwa wananchi ikiwemo boda boda ,mama ntilie pamoja
na wajasiriamali kwa kuanzisha matawi katika maeneo ya masoko .
Leonce amewataka wafanyakazi wa CRDB kutumia vyema siku familia  kwa kukaa
karibu na familia zao na kufurahi pamoja kwani muda mwingi wanautumia
katika kufanya kazi za kuwaingizia kipato .
“Kama kwenye familia mambo hayako vizuri nyumbani hata kazini mambo  hayatakua
vizuri ni vyema kuhakikisha mazingira yanakua mazuri kuanzia kwenye familia
mpaka kazini” Alisema Leons
Kwa upande wake Mteja wa benki hiyo Pendo Shoo amesema kuwa benki hiyo
imemsaidia kuwalipia watoto wake ada kupitia akaunti ya Junior Acount
ambazo huwawezesha pia kupata mikopo kwa ajili ya kuwaendeleza watoto
kielimu.
Benki ya CRDB  ina matawi 8 na matawi mengine madogo madogo bado
yataendelea kuanzisha ili kusogeza huduma za kibenki karibu na wananchi.
Siku ya familia ya CRDB iliambatana na michezo   na burudani  ambazo
zilipamba siku hiyo ikiwemo mchezo wa kuvuta kamba ,kukimbia na yai mdomoni
pamoja na burudani ya muziki .

Post a Comment

0 Comments