WAKATAA KUPANDISHWA KWA BEI ZA MAJI

 Mkurugenzi wa AUWSA, Inj. Ruth Koya akiwa anasoma garama mpya ambapo zilipendekezwa kuongezwa na changamoto walizonazo
 mgeni rasmi wa mkutano huo ambaye ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda wa pili kulia  akiwa na baadhi ya viongozi  waliokaa meza kuu
 picha juu na chini wananchi waliouthuria katika mkutano huo

mmoja wa wananchi  aliyejitambulisha kwa jina la  Ayubu
Mshote akichangia mada
mwananchi wa kata ya sombetini Jenifa Sumaye akiwa
anachangia mada wakati  mkutano wa wadau na watumia
wa maji ulioandaliwa na mamlaka ya huduma na uthibiti wa nishati na
maji (EWURA)uliofanyika katika viwanja vya makumbusho ukiendelea
 Na Woinde Shizza,Arusha

Wananchi wa jiji la Arusha wamekataa kupandishwa kwa gharama za maji
kutokana na kutokuwa na kutokupatiwa huduma bora ya maji na mamlaka ya
maji safi na maji taka(AUWSA) ya jiji hili.

Hayo waliyasema jana jiji hapa wakati wa mkutano wa wadau na watumia
wa maji ulioandaliwa na mamlaka ya huduma na uthibiti wa nishati na
maji (EWURA)uliofanyika katika viwanja vya makumbusho jijini hapa.

Walisema kuwa hawawezi kukubali mamlaka ya maji safi na maji taka
kupandisha gharama za maji wakati huduma ambazo wanazitoa sio nzuri na
hadhikithi maitaji ya wananchi .

Kwa upande wa mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ayubu
Mshote alisema kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikipata faida kila mwaka
lakini wameshindwa kuboresha miundo mbinu yake hali inayofanya kuwepo
kwa tatizo la maji pamoja na upotevu wa maji .

Alisema kuwa faida wanayopata AUWSA ikitumika vyema kwa mahesabu
inaweza kugharamia shuhuli za uendeshaji na uwekezaji  na pia
itasaidia kuweza kubuni vyanzo vipya vya maji vitakavyosaidia
kuboresha huduma za maji na kumfikia kila mwananchi .

Naye Jenifa Sumaye alisema kuwa kumekuwa na tatizo kubwa sana la maji
katika jiji hili hali ambayo inawafanya wananchi kununua maji kwa bei
ghali ,na pia aliitupia mamlaka hiyo ya maji lawana na kusema kuwa
wamekuwa wanakata maji kwa kipindi kirufu halafu wanakuja kusoma mita
na kutoa bili ambayo sio ya kweli.

Kwa upande wake kaimu mwenyekiti wa baraza la ushauri na watumiaji wa
huduma za nishati na maji (EWURA CCC) Mubezi Lutaihwa alisema kuwa wao
hawajaunga mkono upandishwaji wa bei za huduma ya maji kwani mamlaka
hiyo ingebana matumizi na kuongeza ufanisi  katika kutoa huduma na sio
kuwapandishia wananchi gharama.

Alisema kutokana na histori ya upatikanaji wa faida wa AUWSA baraza
alioni kama kunasababu yeyote ya kupandisha bei ya huduma kwa sasa
kwani faida inayopatika inatosha kugaramia shuhuli za uendeshaji n
uwekezaji.

Kwa upande wa mkurugenzi wa AUWSA Eng.Ruth koya alisema Wao  wameamua
kupendekeza kupandishwa kwa gharama za maji ili kuweza  kutoa huduma
bora na kuweza kukarabati miundo mbinu ya maji.

“Tunapandisha gharama hizi ili kuweza kutoa huduma bora pamoja na pia
kwa tumepandisha ili kuweza  kupata hela ya kutatua changamoto
mbalimbali kwani kwa sasa tumeondolew msamaha wa kodi ya ongezeko la
thamani na sasa hivi tunalipia asilimia yote mia moja na pia garama za
umeme zimezidi hivyo tunaongeza ili tuweza kutatua matatizo
hayo”alisema koya
Kwa upande wa kaimu mkurugenzi wa EWURA Nzinyangwa Nchani alisema kuwa
wamepokea maoni kwa ujumla watayafanyia uchambuzi wa kina na kuona
pendekezo lipi linafaa au kitu gani kifanyike na pia watapitia
historia ya mamlaka hiyo na watatoa maamuzi ili wananchi waendelee
kupata huduma bora.

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments :

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia