Bunge
la 11 la Jamhuri ya Muungano linaanza leo Dodoma kwa kusomwa Tangazo la
Rais la Kuitisha Bunge, uchaguzi na Kiapo cha Spika, Kiapo kwa wabunge
wote
Muda
huu tayari wabunge wameanza kuwasili kwenye viwanja vya Bunge na wengi
wamo kantini hapa wakipata staftahi kabla ya kuingia rasmi ukumbini.
Update.
Wabunge wengi wanaingia bungeni now harakaharaka maana mida wowote Kikao kitaanza. Changamoto iliyopo ni kuwa.baadhi ya wabunge hasa wapya wamevaa mavazi ambayo sio ya kibunge jambo ambalo ni kinyume na kanuni. Labda ugeni utawaokoa wasitolewe nje
Wabunge wengi wanaingia bungeni now harakaharaka maana mida wowote Kikao kitaanza. Changamoto iliyopo ni kuwa.baadhi ya wabunge hasa wapya wamevaa mavazi ambayo sio ya kibunge jambo ambalo ni kinyume na kanuni. Labda ugeni utawaokoa wasitolewe nje
Updates
Katibu wa Bunge Dr Kashililah ndio anaanza kwa kusoma tangazo la Rais kuitisha bunge la 11. Mkutano wa uchaguzi unaanza na Andrew chenge anateuliwa kuwa mwenyekiti wa muda kuongoza uchaguzi wa spika. Chenge kaingia na uchaguzi unaanza kwa wagombea kuitwa kujieleza
Katibu wa Bunge Dr Kashililah ndio anaanza kwa kusoma tangazo la Rais kuitisha bunge la 11. Mkutano wa uchaguzi unaanza na Andrew chenge anateuliwa kuwa mwenyekiti wa muda kuongoza uchaguzi wa spika. Chenge kaingia na uchaguzi unaanza kwa wagombea kuitwa kujieleza
Updates
Wagombea wote wameruhusiwa kuingia ndani na wameingia ukumbini isipokuwa Hashim Runngwe ingawa hajajitoa hivyo anaruhusiwa kupigiwa kura bado
Wagombea wote wameruhusiwa kuingia ndani na wameingia ukumbini isipokuwa Hashim Runngwe ingawa hajajitoa hivyo anaruhusiwa kupigiwa kura bado
Updates
Wagombea wametoka nje na wanaitwa mmojammoja kujieleza kwa dakika tatu na maswali matatu kama yapo
==============
Wagombea wametoka nje na wanaitwa mmojammoja kujieleza kwa dakika tatu na maswali matatu kama yapo
==============
Wanaogombania
nafasi ya uspika wanaendelea kuomba kura na sasa ni zamu ya aliyekuwa
naibu spika wa bunge la kumi, Job Ndugai. Amesema anaelimu ya kutosha na
uzoefu pia yeye ni mbunge mwenzao hivyo anaekaa na mgonjwa ndiye
anayejua matatizo ya mgonjwa.
Selasini(Swali): Ni namna gani kama spika utasimamia vyombo mbalimbali vya bunge?
Ndugai: Niwahakikishie taasisi ya bunge naifahamu vizuri ikiwemo vyombo na kamati zake, kwa uzoefu na elimu msiwe na wasiwasi.
Tizeba(Swali):
Ndugai! Tukiacha mambo ya utani kati yangu na wewe, ningependa kujua
uzoefu unaousema mbona haufanani na umri wako, ningependa kujua umri
wako kama hutojali.
Chenge: Hilo sio swali.
Kunchela(Viti
maalum Katavi): Kwa tathmini ya bunge lililopita ulionesha ubabe,
umejipangaje kuendeleza ubabe huo ukipata nafasi?
Chenge: Hilo sio swali, ni maoni yako.
Wabunge wanaomba utaratibu na Chenge anagoma.
Molell: Baadhi ya wabunge walitoka nje bunge lililopita, Ni kwa namna gani atahakikisha bunge hili
Zitto(Utaratibu):
Bunge likishaisha na mambo yake yanaisha, toka maswali yanaanza
mwenyekiti umekuwa unaruhusu maswali kwa reference ya mabunge
yaliyopita.
Chenge: Silichukui hilo la Zitto Kabwe na Ndugai jibu hilo kwa kifupi
Ndugai: Nawahakikishia bunge la amani, umoja na upendo, nawaomba kura zenu, hapa kazi tu.
Anaefuata sasa ni Ole Medeye kupitia CHADEMA
Medeye:
Sheria zinazotungwa na bunge hili ndio msingi wa kugawa haki katika
bunge hili, lengo langu la kwanza nitakalolisimamia ni kuhakikisha
tunapata katiba mpya.
Jambo
la pili natambua wa bunge katika kuisimamia serikali, nitaomba kama
bunge tufanye marekebisho makubwa.(Muda umeisha) Nawaomba kura zenu ili
tuweze kufanya marekebisho hivyo wabunge mnipe fursa, naomba kura.
Bobari(Mchinga):
Natambua mgombea ni mzoefu serikalini, unadhani kasi ya bunge hili
inahitaji spika wa aina gani kuendana na kasi hii.
Medeye:
Wabunge walio wengi ni vijana hivyo mtazamo wa bunge hili ni kesho na
sio jana, nikipewa fursa hiyo nina uwezo wa kusimamia bunge hili, dhima
yangu mojawapo ni kurekebisha bunge.
Nape:
Nakushukuru, naitwa Nape mbunge wa Mtama. Kumbukumbu zinaonyesha
ulishawahi kutolewa na ndugu Lema una tuhuma za ubaguzi, sijui tabia
hizo umeshaacha!
Chenge: Hilo sio swali
Jaffo: Watanzania wamekubali slogan ya Magufuli ya hapa kazi tu, mbunge amejipanga vipi kuhakikisha tunaenda na kasi.
Medeye:
2010 nilinadi ya ari zaidi lakini hatukuenda na kasi hio, tunachotaka
ni serikali kuleta mipango itayoendana na hio Slogan
Wabunge
wote saba waliofika kati ya nane wamejinadi kwa wabunge kasoro Hashim
Rungwe ambae hajafika lakini katibu wa bunge amesema jina lake
litajumuishwa katika wabunge watakaopigiwa kura kwa sababu hajatoa
taarifa ya kujiondoa.
Bunge
limejiridhisha na idadi ya wabunge waliohudhuria kufikia akidi kwani
idadi inayohitajika ili kupiga kura ni nusu ya wabunge wote ambapo
wabunge wote wanaotakiwa ni 364 na idadi ya wabunge waliohudhuria ni
wabunge 359 hivyo kufikisha akidi.
Karatasi
za kupigia kura zinagaiwa kwa wabunge wakiwa kwenye viti vyao na
yanatangwazwa marekebisho kwa jina moja lililokosewa ambalo marekebisho
yake yalishindwa kufanyika ndani ya wakati.
UPDATE:
-->Mh Job Ndugai ametangazwa rasmi kuwa Spika wa Bunge baada ya kupata kura 254
BOFYA HAPA CHINI KUJUA MIKOA AMBAYO MAGUFULI ATAFANYA ZIARA ZA KUSHTUKIZA KUANZIA SASA