Unamkumbuka yule dogo aliyeanzisha redio stesheni yake
nyumbani kwao? Bila shaka umewahi kusoma story yake kwenye kijarida cha kila
mwezi kiitwacho SHUJAAZ ambacho husambazwa na gazeti la Mwanaspoti na vibanda
vya Coca Cola. Sasa hivi, dogo ana habari mpya na njema kwa vijana na wote wanaomfuatilia. Nyota imeanza kung’ara upande
wake na sasa redio kubwa Tanzania EAST AFRICA RADIO imeamua kumpa nafasi aweze
kusikika hewani na show yake mpya iitwayo SHUJAAZ.
“Show yangu itahusika na lifestyle ya vijana kwa ujumla,
bila kusahau burudani kali, story za wana mbali mbali wanaojituma na kutoboa
katika kufikia malengo yao maishani. Pia, utawasikia vijana mbali mbali
wakijadiliana kuhusu ishu zinazowahusu, mfano PESA, MAPENZI, KAZI, MICHEZO,
UJASIRIAMALI n.k, ni lazima tupeane mashavu kama vijana.” Alisema DJ Tee.
Show hiyo itakayoanza rasmi JUMAMOSI hii (07/11/2015) saa
TISA alasiri, inatarajiwa kuvuta hisia za vijana wengi hasa wajasiriamali kwa
kuwa itahusika na ishu zote ambazo zinawahusu vijana kama DJ TEE mwenyewe
alivyoelezea.
Unaweza kupata maelezo zaidi kutoka kwake mwenyewe kwa
kujiunga naye kupitia Facebook jina ni DJ Tee (http://on.fb.me/1FUl1hX),
Twitter (http://bit.ly/1LLGEpK) na
Instagram (http://bit.ly/1Hn07t4)