Mwanafunzi kutoka chuo cha Utumishi wa Umma, Kange,mjini Tanga, Bi.Stella Mwakiliku akiongea na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu vipi wanafunzi wamekikubali kifurushi hicho kilichoboreshwa cha University Pack kutoka Tigo. |
Kikundi cha sarakasi kikitumbuiza wanafunzi katika uzinduzi wa kifurushi cha University
pack kilichoboreshwa katika uwanja wa chuo cha Utumishi wa Umma,Kange, mjini
Tanga. |
Msanii wa kizazi kipya
Roma Mkatoliki akiwatumbuiza wanafunzi wa chuo cha Utumishi wa Umma,Kange,
mjini Tanga,katika uzinduzi wa kifurushi cha University pack kutoka Tigo kilichoboreshwa.
|
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imezindua
kifurushi maalum kinacho wawezesha wanafunzi, ambao ni wateja wa Tigo, kuweza kupigiana
simu bure.
Huduma hii imeboreshwa zaidi baada ya kifurushi
hicho kwa jina maarufu kama Tigo Uni Pack kuzinduliwa mwaka jana, ukilinganisha
na kifurushi cha zamani, kifurushi hichi kipya cha wiki kitawapatia wanafunzi
wepesi wa kujiunga wakiwa popote ndani ya nchi, hii ni kwa mujibu wa taarifa
iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kampuni ya Tigo leo.
Kinachohitajika ili wanafunzi waweze kutumia
huduma hii,ni kuhakiki kwamba wamesajiliwa kama wateja wa Tigo katika Vyou
vyao, ujumbe huo ulisema.
Akizungumzia kifurushi hicho kilichoboreshwa,
Meneja wa Bidhaa kutoka Tigo Edwin Mgoa,alisema kifurushi hicho cha Uni Pack,
kinadhirisha vipi Tigo inavyowasaidia wanafunzi kwa ajili ya kuwawezesha kuweza
kupata huduma za mtandao za maisha ya kidijitali.
Baadhi ya huduma za kidijitali zinazotelewa na
Tigo ni upatikanaji wa muziki bila kikomo kwa kupitia huduma ya Tigo Music,
Facebook ya Kiswahili, Tigo Pesa App, Tigo Backup- huduma inayowawezesha wateja
wa Tigo kuweza kurudisha simu na
zinapoibiwa au kupotea.
Kujisajili
kwa kifurushi cha Uni Pack, mwanafunzi atahitajika kupiga *148*01*20#, namba
ambazo kwa mujibu wa taarifa hiyo, imejumuisha vifurushi vingine muruwa kutoka
Tigo.