MOLLEL ANATOSHA KULIONGOZA JIMBO LA ARUSHA


Na Woinde Shizza,Arusha
Mgombea ubunge wa jimbo la Arusha kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Philemon Mollel amewataka wakazi wa jiji la Arusha kumchagua kwa kura za kishindo kwani anatosha kuliongoza jimbo la Arusha na jiji hilo si sehemu ya kujinadi kwa mapambao bali kuwalete wananchi maendeleo.


Mollel ameyasema hayo wakati alipokuwa akijitambulisha na kuomba kura kwa wakazi wa kata ya Levolosi na kuwataka kuendelea kukiamini chama cha mapinduzi pamoja na yeye kwani anatosha kuliongoza jimbo la Arusha Mjini, wakati chama hicho kijiandaa kuanza kampeni zake hapo Jumamosi ijayo mgombea apita kwenye mashina kuomba kura.


Alisema kuwa anaomba kura kwa wanachama na wasiokuwa wanachama kwani maendeleo hayana itikadi za vyama vya siasa hivyo akawataka kumtuma naye awe mtumishi wa wananchi wa jimbo la Arusha mjini.


“Mnajua siendi kuganga njaa bungeni bali naenda kupeleka kero zenu na nani uchungu na maendeleo ya kinamama,wazee na vijana kwani nitaanzisha saccos kwa kila kata ilimpate mikopo ya kujikwamua na kuweza kujiletea maendeleo”alisema Mollel.


Aliwataka wakereketwa na wale wafuasi wa vyama vingine kuweka pembeni ushabiki na kumchagua yeye ilikuirudiisha Arusha kuwa Giniva ya Afrika na kuirudisha Arusha yenye amani na kuweza kurudisha sifa ya jiji hilo.


Awali akimkaribisha Mgombea kwa wanachama na wafuasi wa chama hicho sanjari na wananchi Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Arusha Dkta Soiley amewakata kuacha ushabiki wa kisiasa na kumchagua Mollel kwani anatosha kuliongoza jimbo la Arusha.


Soiley alisema kuwa pamoja na kupigwa katika uchaguzi mkuu kwa nafasi za udiwani mda umefika kwa kumchagua Philemon Mollel kuweza kuiletea maendeleo na kudumisha sifa ya jiji la Arusha ya kuwa na Amani na kivutio cha utalii kwani uchaguzi ulipita na sasa ni wakati wa kuunganisha nguvu na kumpa kura za kishindo mgombea wa chama hicho.


“Nawasihi ndugu zangu kutafuta wanachama kumi kwa kila mtu ilikuunganisha nguvu na kuipa ccm ubunge wa jimbo letu kwani nyinyi ni mashahidi wakubwa hakuna kilichofanyika katika kuwaletea wananchi maendeleo kwa mda wa mbunge aliyemaliza mda wake kwa kipindi cha miaka mitano”alisema Soiley.

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia