Na Woinde Shizza,Arusha
Wananachi wa jimbo la Arumeru Magharibi wamemuomba mbunge
mteule wa jimbo hilo Gibson
Olemeiseyeki kutatua tatizo la
kero ya maji ambalo linakabili baadhi ya vijiji vya jimbo hilo.
Wamemuomba mbunge huyo mteule kuakikisha anatimiza na kutekeleza ahadi zote ambazo aliziadi
katika kipindi alipokuwa akifanya kampeni ,na sio kuwa kama viongozi waliopita
waliowai kushika nafasi hiyo.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti baadhi ya
wananchi hao walisem a kuwa kumekuwa na desturi ya viongozi wengi kuahidi mambo
mengi wakati wakifanya kampeni lakini wanapopewa nafasi ya kuongoza wanashindwa
kutekeleza ahadi zao.
Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisa kwa jina la Lukas Lomayani
alisema kipindi cha kampeni kimeisha na sasa ni muda wa kufanya kazi na
kuteleza ahadi za wananchi hivyo alimuomba mbunge mteule wa jimbo hilo pamoja
na madiwani kuanza kazi ya utekelezaji.
Alisema kuwa katika jimbo hilo vijiji vingi vimekuwa na
ukosefu wa maji kitu ambacho kimekuwa ni kero kubwa kwa wananchi na kitu
ambacho kimewasumbua kwa muda mrefu kwani viongozi waliopita wamekuwa
wakiwaaadi kuwa watatatua tatizo hilo na badala yake baada ya kupewa kura
wamekuwa wanajisahau na kutofanyia kazi swala hilo.
“unajua wamekuja wengi sana wametuahidi ukiangalia kama mimi natoka katika kijiji cha kiranyi
kijiji hichi kumekuwa na tatizo kubwa sana la maji lakini halipatiwi ufumbuzi
tunateseka sana katika swala hili kwani tumekuwa tunalazimika kwenda kuchota
maji mbali na pia saa ingine imefikia adi haatua ya kununua maji ndoo moja mia
tano hivyo mimi binafsi naomba uyu mbunge jambo la kwanza aanze na kutatua
tatizo la maji katika kijiji hichi cha kiranyi na vijiji vyote ambavyo vinakosa
uduma hii”alisema Seriani Raphael
Naye Prisca Lema kwa kweli sisi wakazi wa kata ya kiranyi tumeteseka sana hususa ni wamama kwani saa ingine tulazimika kufata maji umballi mrefu ata wa kilometa mbili na tukienda uko saa ingine hatupati maji unakuta mwenyewe kaunga au ataki kufungua kwa siku hiyo hivyo iwapo tatizo hili litafumbuliwa tutafurahi mbunge wetu alipokuwa ana pita kuomba kura alituahidikutatua tatizo la maji ambalo linatukabili kwa kipindi cha muda mrefu sasa hivyo tunamuomba aanze na hilo.
Mbunge umteule wa jimbo hilo alipokuwa napita katika kampeni
zake moja ya ahadi aliowahaidi wananchi wake ni kuwaletea maji na alibainisha
kuwa anauwezo wa kutatua tatizo hilo kwani jimbo lake limezungukwa na milima na
vijiji vingi vipo chini yamlima.